Pages

JK, VIONGOZI MBALIMBALI WAMFARIJI MZEE KINGUNGE NGOMALE MWIRU

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya leo. Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa kesho jioni kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Mzee Ally Mtopa.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar es salaam leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwa ameambatana na viongozi Wengine wa Chama hicho waliofika nyumbani wa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kumfariji kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru.
Sehemu ya wanafamilia wakiwa ni nwenye majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)