Pages

TATU MZUKA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUBORESHA NA KULINDA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI

 kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka mwishoni mwa wiki imeadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.
Akizungumza wakati wa shughuli hizo za usafi,Mratibu wa mawasiliano kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka ,Kemi Mutahaba amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa kushirikiana na baadhi ya Wadau kwa kujitolea,lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika suala zima la kuboresha usafi wa mazingira yetu.
"Tumejitolea kufanya usafi
katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,lengo likiwa ni kutunza
mazingira na kuweka mazingira yetu safi, lakini pia ikiwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala zima la kuboresha na kuyaweka mazingira yetu kuwa safi wakati wote",alisema Kemi.
Kemi alisema yote hiyo ni kuhakikisha wanasimamia mlengo wa kampuni yao,waliounzisha katika suala zima la kusaidia kulinda mazingira,ambapo hivi karibuni walichangia kwa kuikabidhi Serikali kiasi cha fedha milioni 100 ili zitumike  katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao Serikali iliishauandaa.
Amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa
kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta
mbalimbali ikiwemo mazingira.

Baadhi ya Wadau na wafanyakazi kutoka kampuni ya
The
Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka wakiadhimisha miaka 56 ya Uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira
mwishoni mwa wiii katika
ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kawe Beach,Kinondoni jini Dar Es Salaam.
Baada ya kumaliza kufanya usafi wakafurahi kwa pamoja
Shughuli ya usafi ilifanyika kw amakini kuhakikisha eneo la Fukwe linabaki safi.
Wadau wa Usafi wakijadilaiana jambo 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)