Pages

SIKU YA TATU YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU KATIKA MLIMA KILIMANJARO KWA WAZALENDO 47 KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU PAMOJA NA KUTANGAZA UTALII WA NDANI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali,George Waitara akiwa katika maandalizi ya kuianza siku ya tatu ya Wazalendo 47 kuelekea katika kilele cha Uhuru ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru .
Baada ya kupumzika kwa muda katikia kituo cha Horombo Wazalendo kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ,Waandishi wa Habari,Marafiki wa China na Tanzania pamoja na Watumishi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) walianza safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo kabla ya kuelekea kilele cha Uhuru.
Safari ilianza kwa Slogan ile ile ya "Mdogo Mdogo"
Baadae Safari ikaingia kwenye barabara yenye mawe hivyo utembeaji katika eneo hili ulihitaji uangalifu wa hali ya juu.
Wengine walitengeneza Tabasamu kuonesha safari itamalizika kwa salama.
Safari iliendelea na kila mmoja alipambana na hali yake.
Hatimaye Wazalendo wakaiacha misitu mifupi bna kuingia katika kituo cha mwisho kabisa yanapotiririka maji.
Hapa Wanapaita "Last Woter Point"
Wazalendo wakafika Last Woter Point na kupata mapumziko ya muda mfupi wakiongozwa na Mwogoza watalii Mkuu,Faustine Chombo kutoka kampuni ya Utalii ya Zara.
Safari ikaingia eneo la mchanga maarufu kama Saddle.hali ya hewa ya eneo hili imekuwa ya kubadiliko kila baada ya dakika chache
Unaweza tembea usimuone mwenzako yupo wapi kutokana na hali ya Ukungu na wakati mwingine mvua ambayo imekuwa ikinyeskatika eneo hilo.
Safari ya muda mrefu ikaelekea katika kituo cha mapumziko cha Kibo Hut.
Wazalendo Wakaingia Kibo Hut kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea kilele cha Uhuru,usiku wa saa tano.
Baadhi ya Wazalendo wakiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Pascal Shelutete wakapata Taswira katika kibao cha Kibo Hut ikiwa ni urefu wa Mita 4720 kutoka usawa wa bahari zikisalia mita 1175 kufika kilele cha Uhuru.
Wazalendo wakipata kumbukumbu katika kituo cha Kibo Hut .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini aliyekuwa katika safari hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)