Pages

SERIKALI KUFANYA MSAKO MKALI KUWASAKA WAAJIRI AMBAO BADO HAWAJAJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Mhe.Anthony Mavunde, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Masha Mshomba, kushoto, wakati akizindua baraza la kwanza la wafanyakazi wa Mfuko huo leo Desemba 22,2017 jijini Dar es Salaam.
NA K-VIS BLOG, FELIX ANDREW
WAAJIRI Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha wafanyakazi  wao  kabla ya  kufanya maamuzi mbali mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi.
Ushauri huo ulitolewa jjini Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira na Vijana , Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC)
Alisema kuwa uongozi shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo. “Lengo kuu la uongozi  shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali mbali na kuzitatua kwa  nia ya kufikia malengo,” alisema. Mavunde aliwaasa wafanyakazi nchini kuondokana  na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa jamii.

“Urasimu katika utoaji wa huduma ni changamoto kubwa sana  ambayo inaisumbua nchi naomba sana msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema. Aidha naibu waziri huyo alisisitiza kwa waajiri wasio jiunga na Mfuko huo kufanya hivyo mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake Alisema kuwa serikali itaanzisha msako mkali mwakani wenye lengo la kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waajiri wote ambao bado hawajajisajili na mfuko huo.

Aliongeza kuwa serikali ilikwisha toa muda wa kujisajili kwa wasiofanya hivyo ambao ulimalizika tarehe 30 Septemba mwaka huu.
Mnamo mwezi Januari mwakani tutaanzisha msako wa kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola waajiri wote  ambao wameshindwa kujisajili na mfuko hadi sasa, alisema

Kwa mujibu wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi namba 263 waajiri wote wanatakiwa kujisajili na mfuko
Sheria inawataka waajiri katika sekta ya umma na binafsi ambao wana  zaidi ya mfanyakazi mmoja kujisajili na mfuko. Kifungu cha 71( 4) cha sheria kinasema kushindwa kujisajili na mfuko ni kosa na endapo itathibitika mwajiri anaweza kutozwa faini isiyozidi kiasi cha shilingi milioni kumi au kifungo cha miaka mitano gerezani.

Kuhusu baraza, alisema kuwa ni muhimu kwa maendeleo  na kuwataka wafanyakazi nchini kuyatumia kwa lengo la kupunguza msuguano sehemu za kazi. “Waaajiri na wafanyakazi wanatakiwa kutumia baraza hili kwa kuleta amani na kuimarisha utendaji kwa maendeleo  ya nchi yetu,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Baraza la Wafanyakazi la WCF Bw Masha Mshomba, alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi katika maamuzi mbali mbali ya kiutendaji  tayari menejimenti kwa kushirikiana na tawi la chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE)  imekamilisha uundaji wa baraza hilo.

Aliongeza kwa mfuko huo umeendelea kutimiza majukumu  yake katika kuchangia maendeleo ya taifa , husani uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuwahudumia wafanyakazi wanoumia au kuugua kutokana na kazi kwa nia ya kuwawezesha kurudi kazini. Aidha mfuko pia unashiriki moja kwa moja katika kujenga uchumi wa viwanda kwa njia  ya ubia na Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini. Katika kusogeza huduma jirani na wadau wote , alisema mfuko umepanga kufungua ofisi zake katika mikoa minne katika robo ya tatu ya mwaka 2017/18

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Arusha , Mwanza na Mbeya huku lengo likiwa ni kuwa na ofisi katika mikoa ishirini. Hadi mwishoni mwa mwezi
Novemba mwaka huu mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2015 ulikuwa umesajali zaidi ya waajiri 12,000 na kulipa fidia kwa  zaidi ya wafanyakazi 280 walioumia na kufariki kutokana na ajali za mahali pa kazi.
Mhe. Mavunde  akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi huo.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba. Kulia mni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la WCF, Bi. Amina Likwangala.
Mhe. Mavunde akizungumza na waandishi wa habari.
Bw.Mshomba akizungumza na waandishi wa habari.
Picha ya pamoja
Bw.Masha akizungumza kabla ya uzinduzi huo
Mhe. Mavunde, (katikati), Bw. Masha Mshomba (kushoto) na Bi Amina Likwangala wakifurahia jambo.
 Mhe. Mavunde, (wapili kushoto) na Bw. Masha Mshomba, (wakwanza kushoto), wakiungana na wafanyakazi kuimba wimbo wa mshikamano.
 Mhe. Mavunde akiongozana na Bw. Mshomba 
 Mhe. Mavunde akipokea Mkataba wa kuunda baraza hilo kati ya uongozi wa WCF na chama cha wafanyakazi TUGHE, tawi la WCF, kutoka kwa Katibu wa Baraz hilo, Bw.Geofrey Masisa.



 Wafanyakazi wa WCF wakiimba wimbo wa mshikamano.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF waliohudhuria hafla hiyo.
Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Anthony Mavunde (wapili toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba (wa kwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa Mfuko mapema leo Desemba 22, 2017 jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la WCF, Bi. Amina Likwangala. Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha
Wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)