Pages

Kamati ya UN kutetea haki za Wapalestina yazungumza na Waziri Dk. Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhiwa kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli alipotembelewa na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisalimiana na Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (wa pili kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika mazungumzo na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akipitia kitabu cha picha na historia ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea mara baada ya kukabidhiwa.
Wanafunzi wa chuo wakiwa kwenye mdahalo na Wajumbe wa Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ilipomtembelea ofisini kwake.

KAMATI maalum ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina imekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kwa mazungumzo maalum walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waziri Dk. Mwakyembe, Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck alisema michezo inaumuhimu mkubwa kwa jamii kwani ni kiungo kinachotumika kujenga mshikamano na kudumisha amani kwa mataifa mbalimbali na jamii kwa ujumla.

Aliwahimiza wanahabari nchini kuendelea kuandika habari za Palestina kiusahihi ili kuielimisha jamii juu ya suala hilo na pia kupaza sauti na hatimaye suluhu kupatikana eneo hilo, aliwataka vijana kupenda kusoma historia za maeneo anuai ikiwemo mvutano kati ya Palestina na Israeli kwa ajili ya kujijengea uelewa wa mambo duniani.

Kwa upande wake

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour akizungumza na waziri alitoa ombi la mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Tanzania na Palestina kudumisha zaidi uhusiano uliopo pande mbili. Kamati hiyo ilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu katika mdahalo, asasi za kiraia na Jukwaa la Wahariri.

Hata hivyo baada ya ziara hiyo na kumtembelea Waziri Dk. Mwakyembe kamati hiyo ilihudhuria maadhimisho ya Siku ya kutetea haki za watu wa Parestina yalioandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)