Pages

BONANZA LA MBUNGE WA SEGEREA LAFANA


Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata  lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali  ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda  ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi  milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata  shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na  shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali  Mheshimiwa Bonnah Kaluwa amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila  mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa  mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo


Wachezaji wa Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)