Pages

BOHARI YA DAWA (MSD) YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KATI 2017-2020

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akihutubia wakati akizindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 wa Bohari ya Dawa (MSD) jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunum akizungumza katika uzinduzi huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa SMD, Sako Mwakalobo, akielezea mpango huo mbele ya mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Wafanyakazi wa MSD na wadau wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo.
uzinduzi ukiendelea.
Wadau na wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Viongozi wa idara mbalimbali wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa pili kulia), Mganga Mkuu wa Serikali, Mohamed Kambi Bakari ( kulia) wakisaini hati ya mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD,  Laurean Bwanakunu ( kulia). Wengine wanao shuhudia tukio hilo ni Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Ilangwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akimkabidhi hata hizo za mkataba Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya, akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD)imezindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020 ili kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. 

Akizindua mpango mkakati huo jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya ameipongeza MSD kwa kuandaa upya mpango huo ambao wamejikosoa na kuboresha maeneo muhimu ili kuendana na vipaumbele vya serikali na mahitaji ya wananchi wa Tanzania, hususan vituo vya Afya vya Umma.

Maeneo hayo muhimu ni pamoja na Kujitegemea kifedha, kuuhuisha Mnyororo wa Ugavi, Kuboresha mfumo wa Tehama, Matumizi yenye tija ya Rasilimali Watu, Utawala na 
Ushirikishwaji wadau.

Katika  hatua nyingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya ameingia mkataba maalumu wa utendaji kazi (Performance Contract)na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu ili kuhakikisha utekelezwaji wa haraka wa Mpango mkakati uliozinduliwa.

Aidha katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema atahakikisha Mpango Mkakati 2017-2020 unatekelezwa ambapo kila Mkurugenzi na Mameneja wa MSD wameingia mikataba inayopimika  ya utendaji kazi. 

Bwanakunu aliongeza kuwa ufuatiliaji wa utendaji utafanywa kupitia Ofisi  maalumu ya kusimamia utekelezaji wa mikakati ya MSD(Strategic Management Office)Tayari kila Mkurugenzi na mameneja wa MSD wamesaini mkataba kutekeleza Mpango Mkakati huo wa Kati.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)