Pages

Benki ya NMB yadhamini Tamasha la 'Mtoto Day Out'

Baadhi ya maofisa wa NMB wakitoa huduma za kibenki kwa washiriki wa Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali katika ukumbi wa Msasani Beach Club, Kawe jijini Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa wa NMB wakitoa huduma za kibenki kwa washiriki wa Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali katika ukumbi wa Msasani Beach Club, Kawe jijini Dar es Salaam. Watoto wakicheza michezo mbalimbali kwenye Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali katika ukumbi wa Msasani Beach Club, Kawe jijini Dar es Salaam.
 
Watoto wakicheza michezo mbalimbali kwenye Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali katika ukumbi wa Msasani Beach Club, Kawe jijini Dar es Salaam.


BENKI ya NMB imedhamini msimu wa pili wa tamasha la watoto 'MtotoDay Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali lililofanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusu ufadhili wa NMB katika tamasha hilo, Kaimu Meneja Mwandamizi Amana na Huduma za Bima NMB, Stephen Adili, alisema wamethamini tamasha hilo ili kuwawezesha watoto kukutana pamoja kufurahi wakiwa pamoja na wazazi wao.

"Sisi kama NMB tumekuwa tukitoa huduma bora kwa ajili ya watoto kwa muda mrefu, zaidi tulikuwa tunaangalia suala la fedha, baadae tukaona ni vyema wapate elimu ya fedha hivyo tukaenda mashuleni kutoa elimu lakini pia tunajua watoto wanapenda kucheza, tukaona leo tushirikiane na Dina Marious kuwakutanisha watoto wakae na wazazi wacheze na kufurahi kwa pamoja.

"Tunatoa elimu kwa mzazi na mtoto kuhusu masuala ya fedha jinsi ya kuweka akiba kwa ajili ya baadae, lakini pia wazazi wakumbuke huu ni mwezi Desemba wajiandae wakijua kwamba Januari kuna majukumu mengi kama ada, sare za shule na gharama zingine," alisema Adili.

Pia Adili alisema katika tamasha hilo kuna huduma mbalimbali za zinatolewa na benki ya NMB ikiwa ni pamoja na kuwafungua watoto na wazazi akaunti, lakini pia kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza fedha kwa matumizi ya baadae.

"Tuna mtoto akaunti kwa ajili ya watoto chini ya miaka 18 inaitwa Mtoto Akaunti, lakini pia tunajua watoto wa miaka 13 hadi 17 tayari wameshajua mambo mengi kwa hiyo tumewatengenezea akaunti yao ambayo yenyewe tunawapa ATM Card na muamala wowote watakaofanya mzazi atapata taarifa,

"Lakini vile vile wazazi ambao hawana akaunti tunawafungia akaunti kupitia ChapChap ambayo unafungua mara moja unapata ATM Card na unaunganishwa na simu banking ambayo itakuwezesha kufanya miamala na huduma zingine za benki kwa kutumia simu," alisema Adili. 
Watoto wakicheza michezo mbalimbali kwenye Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limekutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali katika ukumbi wa Msasani Beach Club, Kawe jijini Dar es Salaam.
 
Wazazi na Watoto wao wakiwa kwenye Tamasha la 'Mtoto Day Out' ambalo limedhaminiwa na Benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)