Pages

VIJANA DAR WATUNUKIWA VYETI BAADA YA KUHITIMU MASOMO YA UFUNDI KUPITIA VSOMO

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akikamkabidhi Cheti Mhitimu wa Mafunzo ya VSOMO kwa njia ya mtandao Sunday Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Airtel Tanzaniam. Kushoto ni Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano.
Meneja wa Mawasiliano wa Airel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya VSOMO Jabir ambayo ni ushirikiano baina ya VETA na Kampuni ya Airtel Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es salaam Bw. Habibu Bukko.

Mamlaka ya mafunzo ya ufundi VETA leo imekabidhi vyeti vya kuhitimu masomo ya ufundi stadi kwa vijana 8 wa mkoa wa Dar es saalam baada ya kuhitimu masomo yao ya ufundi wa umeme wa majumbani pamoja na ufundi wa simu mara baada ya kumaliza kusoma kupitia aplikesheni ya VSOMO na kuhitimu katika viwango vya VETA.

Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es saalam , Bw. Habibu Bukko aliishukuru Airtel kwa ushirikiano wake na VETA kupitia Aplikesheni ya VSOMO ambapo imekuwa ikifaidisha wanafunzi walioko mbali na vyuo vya VETA kuweza kusoma VETA wakiwa popote, vilevile alipongeza vijana hao kwa kutumia simu zao za mkonononi vyema na kuhitimu masomo ya ufundi.

Alisema jitihada hizi za Kufanikiwa kutoa Masomo ya Ufundi stadi kupitia Aplikesheni ya VSOMO zinaenda sambamba na mikakati iliyojiwekea VETA na serikali kwa ujumla katika kutanua wigo ili kutoa wa elimu ya Ufundi stadi hata kwa jamii ambayo bado haifikiwa na miundombinu ya vyuo vya VETA mahali walipo ili nao kuwawezesha kushiriki maendeleo ya jamii.

“Hadi sasa tunao zaidi ya vijana takribani 54 waliohiti masomo yao kupitia VSOMO na kukabithiwa vyeti vyao. “nawapongeza kwa dhati vijana hawa kwa kuhitimu masomo yao leo. Pia tunao wanafunzi 25 wanasubiri kupangiwa masomo ya Vitendo ili kuhitimu na kupata vyeti . Nitoe wito kwao kujiandaa vyema kuingia kwenye mafunzo ya viyendo laikini pia kwa watanzania hususani vijana kutumia fursa hii kujisomea masomo ya ufundi kwa kupitia mfumo huu wa VSOMO wakiwa popote VETA itawahudumua” alisema Bw. Bukko.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)