Pages

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WATEMBELEA HIFADHI YA SELOUS KATIKA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wametembelea katika hifadhi ya ya Taifa ya Selous ili kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA.

Akizungumza mwenyekiti wa umoja huo, Dkt. Liggyla Vumilia alisema kuwa wameamua kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - SELOUS-MATAMBWE, MOROGORO.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Ilikuwa ni furaha kila kona.

Treni ya TAZARA ikichanja mbuga.
 Mahojiano yakiendelea ndani ya treni.
 Moja ya pango ambao treni inapita.
 Reli ya TAZARA imenyooka.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
 Makaribisho ndani ya hoteli iliyopo nje kidogo ya hifadhi ya Selous eneo la Kisaki.
 Wakipata chakula cha usiku.
 Nami mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kulia) niliweza kuwakilisha vyema na wana-CAAT. Pembeni yangu ni Chris na Yusuph.
 Wazee wa kazi Kaijage (mbele) akiwa na Dr. Heri.
 Wana-CAAT wakipata kifungua kinywa.
 Wana-CAAT wakiwa tayari kuingia mbugani kujionea vivutio mbali mbali.

Wana-CAAT wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuingia mbugani.
 Moja ya wanyama wanapatikana hifadhi ya Selous.
 Eneo la Matambwe gate.
 Furaha baada ya kufika eneo la geti kuu.
 Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole akitoa maelezo machache juu ya hifadhi ya Selous.

PORI la akiba la Selous ni moja kati ya hifadhi zenye utajiri wa vivutio adimu vya utalii na ambavyo vinapaswa kutangazwa zaidi kwa ajili ya watalii wa ndani na wa nje.

Selous ni pori la akiba lenye ukubwa wa kilometa za mraba 54,000 likijumuisha maeneo ya ardhi oevu, misitu ya miombo, tambarare, nyasi za kuvutia, maziwa na mito inayotiririka, vyote vikifanya vivutio vya aina yake mbali na wanyama wa aina mbalimbali. Pori hili la akiba la Selous lilianzishwa mwaka 1896 na Wajerumani likiwa ni pori la kwanza kutengwa kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori katika Bara la Afrika na la pili duniani kwa ukubwa baada ya hifadhi ya pori la Marekani ambalo linaitwa Yellowstone. Poro hili limegawanyika katika kanda 8 kiutawala.

Umaarufu wa Selous si katika wanyama pekee ambao ndiyo kivutio kikubwa cha utalii wa uwindaji, utafiti umebaini kuwa katika eneo la Selous kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya mimea ambayo ikitambuliwa na kutangazwa inaweza kuwa kivutio adimu na cha kipekee cha kitalii.
 Wakisoma ramani mbali mbali inayoonyesha hifadhi hiyo.
 Moja ya ramani.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT), Dkt. Liggyla Vumilia akizungumza machache na Mhifadhi wa Wanyama Pori wa Selous kanda ya Matambwe, Gregory Kalokole.
 Moja ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi ya Selous.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)