Pages

Tunakumbushana #SiUchochezi (Kipindi cha kwanza)

Kipindi cha Tunakumbushana #SiUchochezi ni kipindi kipya cha kila wiki kinacholenga kuibua na kuonyesha masuala mbalimbali katika jamii ambapo kitakuwa katika  mfumo wa sauti, picha mnato pamoja na picha jongefu (video).

Kipindi hiki kimejikita kukosoa, kuonya na kusifia masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii yakiwemo ya  kiutendaji, kisiasa, kiuchumi pamoja na kijamii nchini Tanzania.

Kinaandaliwa na kurushwa na mitandao  ya kijamii ya Binagi Media Group (www.bmghabari.com) pamoja na mitandao mingime rafiki kote  nchini, lengo likiwa ni kuamsha ari ya kimaendeleo katika jamii.

Rai ni kwa wadau wote wapenda maendeleo kuungana na BMG katika kuhakikisha kipindi hiki ambacho kimeanza kuruka hewani kwa mara ya kwanza hii leo Novemba Mosi, 2017 kinaleta matokeo  chanya katika jamii.

Binagi Media Group
www.bmghabari.com
0757 43 26 94
Mwanza
#PamojaDaima!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)