Pages

TATU MZUKA YAMPONGEZA BI. BUJINGINYA KUTOKA NGARA KWA KUSHINDA MILIONI 50.

Pichani kulia ni Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera akizungumza jana jijini Dar mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyoibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka  ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki.Pichani kati ni
mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwa pamoja na Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68 kupitia droo ya kila saa.
Pichani kati ni mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akiwatambulisha Washindi wa mchezo  huo,mbele ya Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar.
Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi Bi.
Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera alieibuka  mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka
ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika mwishoni mwa wiki




Mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba akimkabidhi mfano wa hundi,
Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68
kupitia droo ya kila saa.


Judith Bujinginya mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera
ameibuka mshindi wa jackpot ya Tatu Mzuka
ya shilingi milioni 50 katika droo ya 15 iliyofanyika jumapili.

Bi Bujinginya, mama wa watoto wawili ambaye anaungana na
washindi milioni 130  wa Tatumzuka
amesafirishwa kwa ndege kutoka Ngara kuja Dar es Salaam ili kuchukua pesa yake
ya ushindi  katika mkutano na waandishi
wa habari uliofanyika leo Mikocheni.

 Baada ya kushinda mara chache
katika droo ya kila saa, alipata msukumo wa kuendelea kucheza bila kukata
tamaa. "Baada ya kuishi kwa kutafuta pesa ya mlo kila
mwezi na miezi mingine bila pesa, Kiukweli sikujua itakavyokuwa ikifika Januari.
Nimefurahi sana kwamba sasa naweza kutembea kwa kujiamini tena baada ya ushindi
huu’ alikiri Bi Bujinginya.

Pia katika tukio la kukabidhi zawadi kwa mshindi
alikuwepo Bwana Joseph Kofia ambaye alishinda kimaajabu shilingi milioni 68
kupitia droo ya kila saa.Dhamira ya Tatu Mzuka ya kubadilisha maisha ya watu haijabadilika
ambapo zimebaki siku chache ili ichezeshwe droo kubwa ya Supa Mzuka jackpot ya
milioni 150 jumapili ijayo. Tarehe 19 Novemba saa 3:30 usiku Mtanzania mmoja
ataondoka na kitita cha milioni 150.

"Kila mtu ambaye umecheza tangu Tatumzuka izinduliwe
na kutumia kuanzia shilingi 500 tu kupitia MPESA, TIGO PESA au AIRTEL MONEY,
umeingia katika droo hii ambapo unaweza kujishindia milioni 150,"
alielezea mwakilishi wa Tatu Mzuka, Kemi Mutahaba.

Bi Mutahaba aliwahimiza watanzania kuendelea kucheza, akisisitiza
kwamba bado washiriki hawajachelewa kujiwekea nafasi ya ushindi huo wa kihistoria.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)