Pages

NMB kukopesha Nyumba kwa wateja na wasio wateja wao

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (katikati) akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa kampeni maalumu ambayo inatoa fursa kwa wateja wake na wahitaji wasiowateja wa benki hiyo kupata mikopo nafuu ya nyumba. Kulia ni Meneja mikopo ya nyumba Benki ya NMB, Bi. Miranda Lutege. Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (katikati) akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa kampeni maalumu ambayo inatoa fursa kwa wateja wake na wahitaji wasiowateja wa benki hiyo kupata mikopo nafuu ya nyumba. Kulia ni Meneja mikopo ya nyumba Benki ya NMB, Bi. Miranda Lutege pamoja na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi Benki ya NMB, Ally Ngingite wakishuhudia. Meneja mikopo ya nyumba Benki ya NMB, Bi. Miranda Lutege (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kampeni ya mikopo ya nyumba. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga.

BENKI ya NMB leo imezinduwa kampeni maalumu ambayo inatoa fursa kwa wateja wake na wahitaji wasiowateja wa benki hiyo kupata mikopo nafuu ya nyumba. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga alisema mikopo hiyo ya haraka na nafuu inamwezesha mteja kukopa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 10 hadi kufikia milioni 700 huku akiwa na muda wa miaka hadi 15 kufanya marejesho.

Alisema mteja anaweza kukopa ili anunue nyumba, kukopa ili amalizie nyumba yake iliyokwama na hata kutumia nyumba yake kama dhamana na kupewa fedha hadi asilimia 80 ya thamani ya nyumba yake zitakazo msaidia kwa shughuli mbalimbali kulingana na mahitaji yake. Alisema mikopo hiyo nafuu imekuja ili kumaliza changamoto ambazo walikuwa wakiipata Watanzania kwenye ujenzi wa nyumba.

"...NMB inajua makazi ni muhimu sana kwa mwanadamu yeyote na tumeona namna watu wengi wanavyopata changamoto anuai katika ujenzi ndio maana tumekuja na ofa hii na mikopo ya masharti nafuu ya nyumba," alifafanua Omari Mtiga.

Aidha alisema kwa mikopo yakununua nyumba NMB inaweza kumpa mkopo muhusika hadi asilimia 90 ya thamani ya nyumba na kulipia kisha mnunuzi kuchangia asilimia 10 tu. Na wenza wawili (mke na mume) wanaweza kuchukua m kopo wa pamoja kwa kuunganisha vipato vyao vya mwezi kisha kununua nyumba na kuendelea kukatwa taratibu kila mwezi kwa hadi miaka 15.

Mikopo hiyo imeshushwa riba hadi asilimia 17 huku kukiwa hakuna gharama za uendeshaji, kampeni inayoanzia tarehe 1/11/2017 hadi 31/03/2018 hivyo kuwataka wateja wa NMB na wananchi wengine kutumia vema fursa hiyo ya kujikwamua kimakazi na fedha kwa shughuli mbalimbali. Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi Benki ya NMB, Ally Ngingite akifafanua jambo katika uzinduzi wa kampeni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga akifuatilia. Sehemu ya wanahabari wakiwa katika uzinduzi wa kampeni maalumu ambayo inatoa fursa kwa wateja wa Benki ya NMB na wahitaji wasiowateja wa benki hiyo kupata mikopo nafuu ya nyumba.

BENKI ya NMB leo imezinduwa kampeni maalumu ambayo inatoa fursa kwa wateja wake na wahitaji wasiowateja wa benki hiyo kupata mikopo nafuu ya nyumba. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja binafsi wa Benki ya NMB, Omari Mtiga alisema mikopo hiyo ya haraka na nafuu inamwezesha mteja kukopa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 10 hadi kufikia milioni 700 huku akiwa na muda wa miaka hadi 15 kufanya marejesho.

Alisema mteja anaweza kukopa ili anunue nyumba, kukopa ili amalizie nyumba yake iliyokwama na hata kutumia nyumba yake kama dhamana na kupewa fedha hadi asilimia 80 ya thamani ya nyumba yake zitakazo msaidia kwa shughuli mbalimbali kulingana na mahitaji yake. Alisema mikopo hiyo nafuu imekuja ili kumaliza changamoto ambazo walikuwa wakiipata Watanzania kwenye ujenzi wa nyumba.

"...NMB inajua makazi ni muhimu sana kwa mwanadamu yeyote na tumeona namna watu wengi wanavyopata changamoto anuai katika ujenzi ndio maana tumekuja na ofa hii na mikopo ya masharti nafuu ya nyumba," alifafanua Omari Mtiga.

Aidha alisema kwa mikopo ya kununua nyumba NMB inaweza kumpa mkopo muhusika hadi asilimia 90 ya thamani ya nyumba na kulipia kisha mnunuzi kuchangia asilimia 10 tu. Na wenza wawili (mke na mume) wanaweza kuchukua mkopo wa pamoja kwa kuunganisha vipato vyao vya mwezi kisha kununua nyumba na kuendelea kukatwa taratibu kila mwezi kwa hadi miaka 15.

Mikopo hiyo imeshushwa riba hadi asilimia 17 huku kukiwa hakuna gharama za uendeshaji, kampeni inayoanzia tarehe 1/11/2017 hadi 31/03/2018 hivyo kuwataka wateja wa NMB na wananchi wengine kutumia vema fursa hiyo ya kujikwamua kimakazi na fedha kwa shughuli mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)