Pages

Huyu ndio Komando Cairo, Mbwa aliyefanikisha kifo cha Osama Bin Laden

Cairo Akiwa amebebwa na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Marekani.
Mbwa aina ya Belgian Malinois aitwaye Cairo ambaye alikuwa ni Canine Comando katika Kikosi cha Jeshi la Marekani kijulikanacho Kama US Seal Team Six ambacho kilifanikisha mauaji ya Gaidi Osama Bin Laden
Cairo ni moja ya mbwa ambaye alikuwa ni komando katika Kikosi cha US Navy Seal Team Six ambaye alifanikisha Kuuliwa kwa Osama Bin Laden katika operesheni iliyofanywa na Jeshi la Marekani Nchini Pakistan.

Majeshi Mengi ya Nchi karibia zote Duniani hutumia Mbwa kwa kazi mbalimbali kama vile kutuliza Ghasia, Kunusa Mabomu, Kusafisha Njia, Kulinda Viongozi nk. Mbwa wapo wa aina nyingi sana lakini Kawaida tumezoea kuona mbwa aina ya Germany Shepherd katika Vikosi vingi vya Majeshi ya Nchi Nyingi lakini Miaka ya Hivi karibuni tumeanza kuona aina tofauti ya Mbwa inayotumika katika Shughuli mbalimbali kama kwenda vitani na aina hio ya Mbwa inajulikana kama Belgian Malinois. Wa marekani Wanapenda Kusema "A Dog of War" maana yake mbwa wa Vita.

Moja ya aina ya Hii ya Mbwa aina ya Belgian Malinois ndio mbwa aitwaye Komando Cairo (Canine Comando) ambae alikuwa kwenye Kikosi Cha Jeshi la Marekani kiitwacho twenty-three Navy SEALs from Team Six.

Kikosi hiki cha Jeshi la Marekani kilikuwa kikimtumia mbwa huyu aina ya Belgian Malinois katika operesheni ya Kumsaka Gaidi Osama Bin Laden, Mbwa huyu ni kati ya mbwa mwenye akili sana na ambaye amepatiwa mafunzo ya hali ya juu Huku akiweza kupita chini ya Kamba (Slide) na kuruka urefu wa futi 5000 kwenda juu.

Mbwa huyu aina ya Beligian Malinois Ni moja kati ya mbwa ambao kwa sasa dunia ya Kwanza wameanza kuwatumia katika shughuli mbalimbali za kijeshi kama vile Polisi na Jeshi na kutokana na uwezo wao wa kufanya shughuli nzito ndipo hapo wanapojichukulia alama za ushindi tofauti na Mbwa aina ya Germany Shepherd ambae mwanzoni alikuwa akitumiwa katika Majeshi nchi Mbalimbali.

Cairo ambae alitumikia Jeshi la Marekani katika Kikosi kijulikanacho kama twenty-three Navy SEALs from Team Six.

Kazi kubwa ya Mbwa huyu kattika operesheni ya Kumuua Osama Bin Laden ilikuwa ni Kusafisha Njia hususani kwenye Majengo, Kunusa Mabomu, na kunusa sehemu ambapo kuna milango iliyojificha na kuta za kughushi ambapo Osama alihisiwa kuwa angetumia njia hizo.

Cairo alifaliki Mnamo mwaka 2016 akiwa na umri wa Miaka 12 huku akiwa amtunukiwa medali mara baada ya kumaliza Operesheni ya Kumuua Osama Bin Laden ambapo medali hizo zilitolewa kwa kikosi kilichoshiriki katika Operesheni ya Kumuua Osama na Rais Wa Marekani wa Kipindi Barack Obama katika Sherehe za Kuwatunuku Mashujaa hao alitamani kumuona Mbwa Aliyehusika katika Kikosi hiko kijulikanacho kama twenty-three Navy SEALs from Team Six..

Huyo Ndio Cairo the Canine Comando ambaye alihusika Katika Operesheni ya Kumuua Osama Bin Laden

Kwa habari mbalimba kuhusiana na Mbwa, Utunzaji, Kununua, Lishe, Mazoezi Basi usisite kutembelea Tovut yetu ya www.dogtipstanzania.blogspot.com na Ukurasa wetu wa Instagram @dogtipstanzania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)