Pages

ESRF YAWEZESHA WARSHA YA ANDIKO THABITI LA UTAFITI


Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewezesha warsha ya siku 3 kuwajengea uwezo watafiti wa ndani waweze kuandika andiko bora la kuombea fedha kwa ajili ya tafiti.

Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (International Development Research Centre-IDRC) kupitia Jukwaa la Wanazuoni Wabobezi (Think Tank Initiatives), ilifanyika makao makuu ya ESRF, Dar es salaam.

Akizungumza Jijini hapa, Mtalaamu Mwandamizi wa Programu ya Think Tank Initiatives anayeshughulikia Sera za Uchumi, Dkt. John Okidi kutoka (IDRC), amesema kwamba watafiti kutoka nchini za Senegali, Tanzania, Uganda, Ghana na Kenya walikutana kwa siku tatu kujadili na kubadilishana mawazo namna ya kujenga uwezo katika kuandika maandiko thabiti ya kuomba fedha kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa. Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko bora ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia Taasisi ya Kimataifa ya Wanazuoni (Think Tank Initiatives-TTI) na kumalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna umuhimu wa kufanya andiko linaloeleweka ili kuweza kushawishi watoa ruzuku kutoa fedha za utafiti ili kuharakisha mapinduzi ya viwanda nchini.

“Watafiti lazima wawe mstari wa mbele katika kushawishi wanasiasa na viongozi kutegemea zaidi tafiti katika kuleta matokeo chanya kwa wananchi na kusukuma umuhimu wa kutumia tafiti katika kufanya maamuzi kwenye ngazi zote za maamuzi,” aliongeza Dkt. Okidi

Alisisitiza umuhimu wa utafiti katika utungwaji wa sera za maendeleo ya kiuchumi hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inafanya mageuzi makubwa ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda. Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifungua warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kwamba Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo-IDCR ina programu ya miaka kumi ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2019.

Alisisitiza kwamba bila tafiti bora na makini ni vigumu kuwa na sera bora zaidi katika utatuzi wa changamoto za binadamu katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya vijijini.

Dkt. Okidi amesema kwamba watafiti wana umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kwenye ukuaji wa sekta nyingi kama vile gesi, mafuta, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji katika kuongeza tija na mafanikio ya uhakika baada ya matokeo ya utafiti. Picha juu na chini ni Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Uwezeshaji Maendeleo Afrika, Prof. Olu Ajakaiye akielezea namna bora ya utengenezaji wa maandiko kwa ufupi na kwa usahihi wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kwa washiriki kutoka shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana iliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC) kupitia program ya TTI , Julie LaFrance, amesema kwamba ni muhimu kwa watafiti kuendelea na utafiti endelevu na wa kina ili kuweza kuleta matokeo chanya kwa jamii ya watu baada ya kupata matokeo baada ya utafiti.

Aliongeza kwamba baada ya semina hiyo watafiti wa ndani watakuwa wamepata uelewa mkubwa wa kuandika mapendeko thabiti na bora zaidi yenye kuvutia wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kuanza kuwapa fedha kwa ajili ya tafiti zenye tija nchini.

Warsha hiyo pia iliwakutanisha watafiti kutoka Taasisi ya IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na chuo cha Jamii kutoka Ghana.

Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akiwasilisha mada umuhimu wa jinsia kama moja ya kipengele muhimu katika kuandaa maandiko mbalimbali ya kitafiti katika kushawishi wabia wa maendeleo kutoa ruzuku za uatfiti.
Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance akifurahi jambo wakati mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akichangia jambo wakati wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI. Prof. Peter Okidi-Lating (aliyesimama) kutoka Chuo Kikuu cha Makerere akipitia meza za vikundi kazi vya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI. Mtaalamu wa Uwezeshaji Jinsia, Maureen Miruka akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa zoezi la vikundi kazi katika meza ya washirki kutoka ESRF katika warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Pichani juu mshiriki Aldegunda Ngowi kutoka ESRF na chini ni mshiriki kutoka Ghana wakichangia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo.

Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki wa warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku kutoka Shirika la IPAR- Senegal, Taasisi ya Takwimu, Jamii na Utafiti wa Uchumi (ISSER), REPOA, ESRF, STIPRO na Chuo cha Jamii kutoka Ghana.

Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akibadilishana mawazo na Mtalaamu Mwandamizi wa Uwezeshaji Maendeleo na Mafunzo wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Maendeleo (IDRC), Julie LaFrance wakati warsha ya siku tatu ya uwezeshaji wa maandiko ya utoaji ruzuku iliyoandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa IDCR kupitia Think Tank Initiatives-TTI.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)