Pages

DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAKABIDHI CHUMBA CHA MAKTABA SHULE YA MSINGI MUUNGANO

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke, Bakari Makele  akizungumza wakati wa makabidhiano ya Makataba iliyokarabatiwa na kwa shule ya Msingi Muungano  iliyopo Manispaa Temeke jijini Dar es Salaam yaliyofanyika leo 


Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akionesha moja ya kitabu alipokuwa anazungumza na wageni waalikwa, walimu na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa maktaba iliyokarabatiwa na Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwenye shule ya msingi Muungano.
Mwalimu Mkuu ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo akisoma risala kwa mgeni rasmiwakati wa zoezi la uzinduzi wa maktaba shuleni hapo leo. wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Temeke, Bakari Makele.
Mwakilishi Taasisi ya Sema-Tanzania Itanisa Mbise akizungumza wakti wa uzinduzi wa maktaba katika shule ya msingi ya Muungano pamoja na kumkabidhi Dada Mkuu wa shule Veronica Mruma nakala 100 za jarida linalochapishwa na Taasisi hiyo kwa matumizi ya maktaba hiyo.


Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Muungano waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.


Dada mkuu wa Msingi ya Muungano, Veronika Mruma akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa ufunzi wa maktaba iliyokarabatiwa na  Dr. Ntuyabaliwe Foundation leo.
Wanafuzi wakifanza igizo
Baadhi ya wageni waalikwa, wanafunzi pamoja na walimu wakifuatlia mada kwenye uzinduzi wa maktaba katika shule ya msingi ya Muungano iliyopo Manispaa Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akikata utepe kuashiria uzikizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo katika shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akipongezwa mara baada ya kuonesha muonekano wa awali(kwenye picha) kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo(kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu ya Msingi ya Serengeti, Daudi Sabai(Kushoto).
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao.

Taasisi ya Dr Mtuyabaliwe imekabidhi Chumba cha maktaba, ilichokikarabati na kukisheheni vitabu, kwa shule ya Msingi Muungano iliyopo Manispaa Temeke, ambayo tangu kuanzishwa kwake miaka 30 iliyopita  haikuwahi kuwa na maktaba.

Akikabidhi Maktaba hiyo Mkurugenzi na Muasisi wa Taasisi ya Dr Ntuyabakiwe Jacquiline Mengi amesema Taasisi hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2015 kumuenzi marehemu baba yake aliyekuwa mpenzi mkubwa wa kusoma vitabu, inahimiza usomaji wa vitabu kwa wanafunzi,ikiwa ni kuunga mkono  jitihada za serikali za kutoa elimu bora nchini:
Katika salaamu zao za shukrani Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa Bw. Bakari Makele, Mwalimu Mkuu Esther Matowo na Dada mkuu Veronika Mruma wameshukuru kwa msaada huo na kuahidi kuitunza na kuitumia ipasavyo.

Wakati wa hafla hiyo Mwakilishi Taasisi ya Sema-Tanzania Itanisa Mbise alikabidhi kwa Dada Mkuu wa shule Veronica Mruma nakala 100 za jarida linalochapishwa na Taasisi hiyo kwa matumizi ya maktaba hiyo.
Makabidhiano ya Makataba hiyo kwa shule ya Msingi Muungano yamefanyika wakati ambao Wizara ya elimu imeingiza somo la Maktaba katika mtaala wa elimu baada ya kuona umuhimu wake katika kufanikisha utoaji wa elimu katika shule za msingi.
Dr Ntuyabaliwe Foundation ni taasisi pekee binafsi nchini inayojihusisha na utoaji wa misaada ya vitabu vya maktaba kwa shule za msingi nchini, na hadi sasa imekwishatoa misaada kama huo kwa shule mbili za msingi za jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)