Pages

ASKARI MAGEREZA KUTUKA WILAYA YA TEMEKE ASHINDA DAU KUBWA LA MILIONI 11O ZA TATU MZUKA





Afisa Magereza Bwana Neuro Mbwilo amejishindia dau kubwa kuwahi kutolewa na Tatu Mzuka la shilingi milioni 110 kupitia Mzuka jackpot iliyoonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya runinga nchi nzima siku ya Jumapili ya Tarehe 29 Nov 2017.

Kama ma milioni ya wachezaji wengine nchini Tanzania, Mbwilo alidhani ilikuwa ni fursa nzuri kutumia Shilingi 500 kubadilisha maisha yake pamoja na familia milele.

Bwana Mbwilo, ambaye ni Askari gereza wilayani Temeke alielezea mshtuko wake juu ya bahati iyo iliyomtembelea. "Ni hisia ambayo haielezeki kabisa. Nina furaha kubwa sana, nimejawa na shukrani nyingi,na kwangu hii ni ajabu kabisa ", alielezea mbele ya vyombo vya habari.

Katika kutoa hundi ya ushindi huo wa milioni 110 Bwana Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka alielezea zaidi juu ya ushindi huo mkubwa lakini aliwakumbusha Watanzania kwamba kuna njia nyingi za kushinda kupitia Tatu Mzuka. Alifafanua kuwa katika wiki 13 tu Tatu Mzuka imetengeneza zaidi ya washindi milioni 2 na kutoa billion 4 kwa washindi.

Watanzania wanachokipenda kuhusu Tatu Mzuka sio mzuka jackpot tu ya kila wiki lakini pia ukweli kwamba kila ukicheza inakupa nafasi ya kushinda hadi milioni sita kila saa" alisema Maganga

"Mambo yanavutia zaidi mwezi huu ambapo unaweza kushinda kila saa, kuingia kwenye droo ya ‘Jackpot’ ya Jumapili ambayo dau lake ni Milioni 60 wiki hii , na zaidi ya hapo ukicheza unapata nafasi ya bure ya kuingia kwenye droo kubwa yenye dau la kuvunja rekodi la Tshs 150million ya Supa Mzuka Jackpot itakayofanyika Novemba 19 mwaka huu ".

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bwana Felix Lyaniva ambaye alihudhuria mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi yake leo alizungumzia kuhusu matokeo chaya ya ushindi huo kwenye wilaya yake.

"Afisa Mbwilo, sasa umekuwa balozi wa Tatu Mzuka katika Wilaya yangu. Natumaini utatumia fursa hii kubadili maisha ya watu wengine kama ambavyo Tatu Mzuka imebadilisha yako kwa kutumia vizuri mamilioni uliyojishindia. " alisema Mheshimiwa Lyaniya.

Ingawa maisha yake yamebadilishwa milele, Afisa Mbwilo anapanga kuendelea kufanya kazi yake, akisisitiza kwamba ni mshahara wake ndio uliompa nafasi ya kucheza na kushinda.
 Mshindi wa millioni 110 Bwn. Mbwilo akiwa na washkaji zake wawili Juma
Athuman na Joseph Haule Walio zawadia  milioni moja moja na Tatu Mzuka
kwenye promotion ya "Cheza na Washkaji na Shinda na Washkaji".
  Bwana Mbwilo akisherekea ushindi wake na Mke wake Nyumbani kwao Keko.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva ( Kushoto)  akimkabidhi Mfano wa
hundi ya sh Milioni 110 Ofisa wa Jeshi la Magereza Neuro Mbwilo, ambaye
ni mshindi wa bahati nasibu ya Mzuka jackpot, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)