Pages

AIRTEL YAIMARISHA MAWASILIANO KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe 29/11/2017
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (katikati), akipokea msaada wa simu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Aitel Tanzania Bi. Beatrice Singano (kushoto), katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe 29/11/2017 
 Kamishna wa Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari, Maafisa wa Zimamoto na Uokoaji na Wafanyakazi wa Airtel, katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe 29/11/2017.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (Kulia), Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano (katikati) wakishika kipeperushi kinachoonyesha namba ya dharura 114 ya Jeshi. katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo tarehe 29/11/2017
Picha ya Pamoja, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa pili kulia) akiwa na Maafisa waandamizi wa Jeshi hilo pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano (wa tatu kulia), katika makabidhiano ya msaada wa simu zitakazotumika kwenye namba ya dharura 114 yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam leo (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji).

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Airtel Tanzania imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatumika kwa ajili ya kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya dharura 114 wakati wa kutoa taarifa za dharura za moto na majanga mbalimbali nchini.

Simu hizo zimetolewa kwa Mikoa yote ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure ilikupata huduma za Jeshi hilo. 

Akikabidhi simu hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema wao kama Airtel wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi sasa wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya dharura.

“Airtel tunatambua umuhimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika jamii, hivyo tunaamini utoaji wa taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji na kuzuia kwa kiwango kikubwa hasara ambayo inaweza kusababishwa na majanga hayo katika jamii” alisema Mkurugenzi huyo.

Kwa Upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Thobias Andengenye aliishukuru Kampuni ya Airtel kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano kwa msaada huo wa simu na kusema utaimarisha utendaji wa Jeshi hilo.

Wateja wa Airtel sasa wataweza kupata huduma kwa haraka baada ya kupiga simu. “Tunashukuru sana na tuna imani kuwa wateja wa Airtel sasa watakuwa na urahisi wa kutufikia kupitia namba 114, tofauti na hapo nyuma” alisema Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo

Natoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia vema mitandao ya simu kwa kutolea taarifa za kweli na si vinginevyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mwananchi yeyote atakayetumia vibaya mawasiliano ya kimtandao, hasa kwa kuitumia vibaya namba ya dharura 114 inayotumiwa na wananchi kutolea taarifa za matukio ya moto, maokozi na majanga mengine.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)