Pages

WAZIRI WA MALIASILI DKT. KIGWANGALLA AWASILI DODOMA, ATETA NA WATUMISHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Oktoba 21,2017 amewasili Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii Mjini Dodoma na kufanya mkutano na watumishi pamoja na wakuu wa taasisi ya Wizara hiyo.

Awali akiwasili Wizarani hapo, Waziri Dk. Kigwangalla alipata kupokelewa na viongozi wakuu wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu Aloyce Nzuki pamoja na Naibu Waziri Japhet Hasunga (MB) na kisha kutembezwa kwenye ofisi mbalimbali za wizara hiyo.

Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Waziri Dkt. Kigwangalla aliwataka watumishi wote kuzingatia miiko ya kazi kwa kila mmoja kusimama kwenye nafasi yake kama mtumishi aliyehaminiwa na Serikali.

“Kwa pamoja tushirikiane kuijenga Wizara hii kama dhamana tuliopewa na Mh. Rais wetu. Sisi tumekuja hapa kusimamia yale yote ya dhana na malengo kusogeza mbele gurudumu la wizara hii.

Tunahitaji sana uzoefu wenu, ufanisi wenu kwani mutaongeza spidi kwa kila mmoja wenu..aliyekuwa anakamata majangili 5, aongeze juhudi akamate 10 ama zaidi,

Aliyekuwa analeta watalii wachache aongeze bidii alete wengi zaidi na wengine hivyohivyo” Dkt. Kigwangalla alisema wakati akiteta na watumishi hao.

Pia aliwataka wataalam wote kuzingatia ufanisi wao wa kazi awe Daktari, Profesa ama mzoefu wa muda mrefu basi anahakika watamsaidia katika kuinua Wizara hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali. Gaudence Milanzi amemwakikishia Waziri Dkt. Kigwangalla ushirikiano mkubwa katika kazi.

Aidha, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo wamepata kuwasilisha mada mbalimbali za idara zao na namna ya utekelezaji majukumu yao.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akikaribishwa wizani hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akisaini kitabu cha wageni alipowasili ofisini hapo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha wageni wageni kwa Ofisi ya Waziri wa Wizara hiyo katika Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma. kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Aloyce Nzuki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla wakati alipowasili ofisini hapo Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi akimtembeza kwenye viunga vya Wizara hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla. Wengine watendaji wakuu wa wizara.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakiteta jambo baada ya kuzungumza na Watumishi katika Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla katika mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Maliasili na Utalii, Dorina Makaya akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla kumaliza kuzungumza na Watumishi wa makao Makuu mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangwalla ( katikati ) akizungumza na Watumishi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada kuwasili kwa mara kwanza katika Makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii eneo la Kilimani Barabara ya askari mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)