Pages

WAZIRI KALEMAN ATAKA MADENI YA BILI ZA UMEME KULIPWA KWA WAKATI TANESCO

 WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard  Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na  wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili
kuwezesha
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani
 Wajumbe na wadau mbalimbali wa nishati wakifuatilia kikao hicho leo


 Baadhi ya wajumbe wa uongozi wa  shirika kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uzalishaji Umeme Mhandisi  Abdallah Ikwasa na kushoto ni Meneja wa Mwandamizi wa Tehama Dudu
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanesco nchini  Dkt Tito Mwinuka kushoto  na Mkurugenzi wa REA Mhandisi Gisima Nyamuhanga wakifuatilia kikao hicho
 Baadhi ya wajumbe wa bodi ya  wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakimsikiliza kwa umakini Waziri Nishati,Dkt Medard Kalemani katika kikao hicho
Waziri wa Nishati Dkt Medard  Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha
nishati ya umeme wa uhakika unapatikana. 
Aliyasema hayo leo katika kikao  cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo  alisema  watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika  wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka  zaidi .

Licha ya hivyo lakini pia Waziri  huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi .

Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman  alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani  kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja.

"Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo  vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya  nchi na uzalendo "Alisema.

Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa  wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya  kazi kwa waledi mkubwa

Aidha alisema kuwa mkakati wa  shirika hilo ni kuhakikisha mpaka ifikapo 2020 madeni yote shirika hilo wanayoyadaiwa kwa wateja mbalimbali nchini yatakuwa yamekwisha kulipwa.

Sambamba na hayo alikema vitendo  vya wizi wa umeme na kuwataka wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja na ambao watabainika watachukua hatua.  
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)