Pages

WASHINDI WA PROMOSHENI YA COCA-COLA WAKABIDHIWA ZAWADI

Mshindi wa kitita cha 100,000/-Abdul Khalfan (kulia) akipokea fedha zake kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola,Mwanza,Samwel Makenge
Washindi wa promosheni ya Mchongo chini ya kizibo wakiwa na zawadi zao baada ya kukabidhiwa jijini Mwanza jana.
Mshindi wa Televisheni, Fred Charles akipokea zawadi aliyojishindia kutoka kwa Meneja wa Masoko na Mauzo wa Coca-Cola, Mwanza-Samwel Makenge
.Mshindi Davis Gombanila akikabidhiwa zawadi ya televisheni
Mshindi Rashid Mlobelo akikabidhiwa kitita cha shilingi 100,000/-alizojishindia
---
Promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’iliyozinduliwa na Coca-Cola mkoani Mwanza wiki iliyopita imeanza kuibua washindi ambapo wakazi wawili wa jijini Mwanza wamejishindia Televisheni na wengine 2 kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/-kila mmoja wao.

Promosheni hii inahusisha vinywaji vya Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida na inafanyika mkoani Mwanza na mikoa mingine ya kanda ya ziwa ikiwemo mikoa jirani yake ya Shinyanga na Kigoma na itawawezesha wateja kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure.

Akiongea katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi,alisema lengo la promosheni hii kubwa ni kuwazawadia na kuwashukuru wateja wanaotumia bidhaa za kampuni

“Tumewaletea promosheni hii kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu wote wanaotumia bidhaa zetu kama mnavyoona leo washindi wa promosheni hii wamekabidhiwa zawadi zao,natoa wito kwa wananchi kuzidi kuichangamkia ili kujishindia zawadi kwa kuwa bado kuna zawadi nyingi za kushinda”alisema Kisusi.

Mmoja wa washindi wa TV,Fred Charles mkazi wa kitongoji cha Buzuruga akiongea kwa furaha alisema kuwa hakuamini macho yake baada ya kunywa soda ya Coca-Cola na kukuta ina kizibo cha zawadi ya TV “Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo nimeweza kukabidhiwa zawadi yangu kwa haraka,natoa wito kwa wakazi wa Mwanza tuchangamkie promosheni hii tuweze kujishindia zawadi kama nilivyoshinda mimi”alisema.

Naye Rashid Mlobelo mkazi wa kitongoji cha Nyegezi jijini Mwanza alisema amefurahishwa na zawadi aliyoipata kupitia promosheni ya ‘Mchongo chini ya kizibo’ alisema kuwa fedha alizozipata zitamsaidia kununua mahitaji mbalimbali

Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi ni Davis Gombanila aliyejishindia TV na Abdul Khalfan aliyejishia shilingi 100,000/-

Kisusi,alisisitiza kuwa ili mteja kujishindia zawadi anatakiwa kubandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 “Kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele na zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilivyo zawadi kubwa’’.

Alisema zawadi zote kubwa zitatolewa kwa washindi kiwandani na zawadi ndogondogo zitatolewa kwa mawakala wanaouza bidhaa za kampuni na magari ya usambazaji vinywaji vya Coca-Cola.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)