Pages

WAKAZI WA MWANZA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA HISA


Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Khadija Nyembo akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella.
Rai hiyo imetolewa jana na wataalam wa uwekezaji katika masoko ya dhamana na mitaji walipokuwa wakizungumza na wafanyabiashara, wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma Jijini Mwanza kwenye mjadala ulioandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa ushirikiano na Best Dialogue (Mpango wa Uboreshaji Mazingira ya Biashara nchini)Mjadala huo ulilenga kuangalia fursa na changamoto za biashara zinazoikumba sekta binafsi na namna ya kuzitatua na kuwezesha ustawi wa biashara jijini Mwanza ili kuweza kufikia uchumi wa kati na viwanda.Mgeni rasmi katika mjadala huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Khadija Nyembo ambaye alisema kuwa Serikali iko tayari kuboresha mazingira ya kibiashara ili kufikia uchumi wa kati pamoja na Tanzania ya viwanda.

Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akielezea umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa za jana Jijini Mwanza ambapo mafunzo ya mjadala kati ya sekta ya umma na sekta binafsi yalifanyika.
Akizungumza katika mjadala huo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank ,Ibrahim Mwangalaba alitoa rai kwa wadau wa sekta binasfi, sekta ya umma na wakazi wa Mwanza kuwekeza katika ununuaji wa hisa za Maendeleo Bank ambazo zimeanza kuuzwa tangu Septemba 18 hadi Novemba 03 mwaka huu.Mwangalaba amesema hisa za benki hiyo zinauzwa kwa thamani ya shilingi 600 kila moja na kwamba kiwango cha chini ya ununuzi ni hisa 100 zenye thamani ya shilingi 60,000 hivyo wananchi wote wachangamkie fursa hiyo muhimu.

Wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma wakifatilia mkadala wa uboreshaji wa mazingira ya biashara ulioambatana na umuhimu wa kuwekeza kwa njia ya hisa ulioletwa na Mkurugenzi wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba pamoja na mshauri wa uwekezaji katika masoko ya mitaji Richard Manamba.
Tunauza hisa sokoni sasa na hisa hizi zinauzwa kwenye matawi yote ya benki ya CRDB ambapo tunaunga mkono juhudi za Rais wetu anayesema uchumi wa Tanzania umilikiwe na watanzania wenyewe na njia mojawapo ya kuwajumuisha watanzania wengi ni uuzaji wa hisa sokoni”. Amesisitiza Mwangalaba na kuongeza kwamba hisa hizo pia zinapatikana ofisi za TCCIA.Naye Mshauri wa Hisa, Richard Manamba amesema ununuzi wa hisa una faida nyingi ikiwemo wanunuzi kupata gawio la faida ambalo benki hulipata na kwamba hisa hizo huongezeka thamani kulingana na nguvu ya soko.Maendeleo Bank yenye mtaji wa shilingi bilioni 10 sokoni inaendelea kuongeza mtaji wake hadi kufikia shilingi bilioni 17 ambapo inatarajiwa kufungua matawi yake katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)