Pages

TAARIFA YA MATENGENEZO YA DHARURA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KINYEREZI I

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa Wataalamu wetu wanafanya matengenezo ya dharura katika Mfumo wa kupokea gesi kwenye kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia cha Kinyerezi I.

Hivyo Kituo kitazimwa Saa 6:00 mchana hadi Saa 7:00 Mchana ili kupisha matengenezo. Baadhi ya maeneo mbalimbali ya nchi katika kipindi hicho yatakosa umeme.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-       
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

31/10/2017

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)