Pages

NMB yakabidhi vifaa vya kuhifadhia taka kwa jiji la Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana (wa pili kulia) akiangalia vifaa vya kuhidhia taka alivyokabidhiwa na mameneja wa matawi ya Benki ya NMB ya jijini Dar es Salaam wakati wa hafla iliyofanyika juzi. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Bi. Vick Bishubo. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana (kushoto) akimshukuru Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Bi. Vick Bishubo baada ya kupokea vifaa vya kuhifadhia taka vilivyotolewa na Mameneja wa Matawi ya benki ya NMB ya jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana akisalimiana na baadhi ya mameneja wa matawi ya Benki ya NMB ya Jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuhifadhia taka vilivyotolewa na Mamemeja hao Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana akiwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es salaam na Pwani, Bi. Vick Bishubo mara baada ya zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)