Pages

NMB yaahidi kuzingatia uwiano wa kijinsia kuchochea maendeleo

Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias katika mdahalo kuhusu uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias (wa pili kulia) akizungumza katika mdahalo kuhusu uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni washiriki katika mdahalo huo.

BENKI ya NMB Tanzania imesema licha ya kutoa huduma bora kwa wateja wake itaendelea kuhakikisha inazingatia uwiano wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume ili kuwapa nafasi wote kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha za Kigeni katika Benki ya NMB, Gladness Deogratias katika mdahalo kuhusu uwaniano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking ambao unalengo la kuangalia namna bora ya kuwafikia wanawake katika maeneo mbalimbali duniani ili wapate huduma za kifedha.

Gladness alisema benki hiyo inatambua umuhimu wa kuwa na uwiano wa kijinsia kuanzia kwa wafanyakazi wake mpaka aina ya huduma ambazo wanazitoa kwa wateja wake. Alisema NMB imekuwa na sera bora ambazo zinawapa nafasi sawa wanawake na wanaume katika vyeo mbalimbali vya ofisi, kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo namna wanaweza kufanya ili kufanikiwa na kwa wajasiliamali kutoa mafunzo kuhusu njia bora ambayo wanaweza kuitumia kuendeleza biashara zao.

“Uwiano wa kijinsia katika mashirika ni muhimu ili kuwapa nafasi wanawake washiriki katika shughuli za maendeleo, kwetu NMB wanawake wanapewa nafasi na hii inatokana na benki yetu kuwa na sera bora ambazo zinazingatia uwiano uliopo kwa wafanyakazi wake kuanzia wafanyakazi wetu wa kawaida hadi viongozi lakini pia tuna Jukwaa la Wanawake ambalo linatumika kutuunganisha wanawake,"

“Tumekuwa tukitoa mafunzo katika chuo cha IFM, CBE na UDSM, tunakutana na wanawake na tunawapa historia zetu jinsi tulivyoweza kufanya na kufanikiwa na wapo ambao wanatamani kufanya kazi benki tunawapa mbinu ambazo wanaweza tumia kupata nafasi benki kama unavyojua wanawake wengi wana aibu na hawajiamini hivyo tunawambia nini wanatakiwa kufanya,” alisema Gladness na kuongeza.

“Jukwaa letu la wanawake linafanya kazi kwa karibu na kitengo chetu cha Business Bank ambao wao wanatoa mafunzo kwa Klabu za Biashara (Business Club), wao tumekuwa tukiwaomba watoe limu kwa wajasiliamali wanawake huko mikoani kama unavyojua ukiweza kumkomboa mwanakme kiuchumi umekomboa jamii nzima.”

Gladness alisema changamoto kubwa ambayo inawapata wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na elimu ya namna wanaweza kutunza taarifa zao za kuuza na kununua bidhaa ili wanapokwenda benki waweze kupatiwa mikopo kwa urahisi jambo ambalo Business Club imekuwa ikilitolea mafunzo kwa wajasiriamali.

Aidha Gladness alisema kwa wajasiriamali wanawake benki ya NMB ina akaunti ambayo inatwa Pamoja (Pamoja Account) ambayo inatumiwa na vikundi na hivyo kuwataka wanawake kuitumia akaunti hiyo kwani ina huduma za kisasa ambazo zinaweza kuwasaida kukuza biashara zao na kuinuka kiuchumi.

“Akaunti ya Pamoja ina huduma ambazo hazipo katika akaunti za kawaida, wataweza kuona mahesabu yao vizuri, wanaweza kupata huduma kwenye simu inakuwa sio kama zamani ambapo ilikuwa ukitaka kuchukua mkopo mpaka mweka hazina awepo lakini kwasasa wanaweza kutumia NMB Mobile Banking,” alisema Gladness.
Mdahalo kuhusiana na uwiano wa kijinsia kwenye mkutano wa Women’s World Banking unaofanyika jijini Dar es Salaam ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)