Pages

NDOA YA MENEJA WA GLOBAL PUBLISHERS, ABDALLAH MRISHO YATIKISA DAR (VIDEO)

Meneja Abdallah Mrisho na mkewe, Catherine Mdamu wakiwa katika pozi la furaha, muda mfupi baada ya kufungwa kwa ndoa yao. Meneja Mrisho na mkewe, wakiwa na wanafamilia (walioshika magazeti), wakifurahi kwa pamoja baada ya kufungwa kwa ndoa yao.[ Bibi Harusi, Catherine (katikati) akiwa na wanafamilia (wenye nguo nyeupe) na wafanyakazi wenzake, Women With Voices (WWV) wenye nguo za bluu. Daaab! Maharusi na wanafamilia wakiwa katika pozi maarufu kwa jina la dab! Maharusi wakiwa na wapambe wao, Said Mdoe na mkewe Wakifurahia jambo baada ya kufungwa kwa ndoa yao.

Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, jana (Jumamosi, Sept. 30,2017) alifunga ndoa ya kifahari na Catherine Mdamu, iliyolifanya Jiji la Dar es Salaam lisimame kwa muda, ikifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Katika sherehe hiyo, wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiongozwa na mkurugenzi wao, Eric Shigongo, jamaa na marafiki, walijumuika kula, kunywa mpaka kusaza na kucheza muziki mzuri, mpaka usiku sana huku kukiwa na 'special appearance' ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.

Harusi ya Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 1


Harusi ya Meneja Abdallah na Catherine, Mlimani City - Part 2


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)