Pages

KAMPENI YA 3D YAIPAISHA SHULE JOHN BAPTIST GIRLS SEKONDARI

Mwanafunzi wa kidato cha nne, Doroth Samson akizungumza na waandishi wa habari
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameonyesha kufurahishwa na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu! kuwa imewaongezea morali wa kufanya vizuri darasani. Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wanafunzi hao walisema kampeni hiyo imewasaidia sana katika kufanya vizuri katika masomo yao darasani kwa kile walichodai kuwa kuwa bila ya nidhamu katika jambo lolote hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana. Doroth Samson mmoja wa wanafunzi hao wa kidato cha nne shuleni hapo alisema hawana budi kuupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuzindua kampeni hiyo kwani imewasaidia kuwaongezea nidhamu ya hali ya juu ambayo ni chachu ya kufanya vizuri katika masomo yao. 
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist, Aspiter Kibona akizungumza na waandishi wa habari. 
Akaongezea pia, kutokana na nidhamu "Kwa kweli naweza kuthubutu kusema shule hii ni ya pekee ya wasichana ambayo inaongoza kwa nidhamu ya hali ya juu sana na kizuri zaidi nidhamu iliyopo shuleni hapa si kwa wanafunzi pekee bali ni kuanzia kwa Mkurugenzi, Mkuu wa shule, walimu na wafanyakazi wengine, " alisema Samsoni. Mwanafunzi mwingine wa kidato cha tatu shuleni hapo, Vanessa Kyamasi yeye kwa upande wake alisema anajivunia kusoma katika shule hiyo kwani ina kila sifa inayotakiwa kwa mwanafunzi anayependa kusoma. Kyamasi alisema shule hiyo ni moja ya shule za kuigwa nchini kutokana na nidhamu kubwa iliyopo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo chache inayochangia wafanye vizuri katika masomo yao darasani.. Naye Mkuu wa shule hiyo, Aspiter Kibona lengo la kampeni hiyo ni kumkomboa mtoto wa kike katika kuhakikisha anafanya vizuri katika masomo yake darasani. Kibona alisema waliamua kuzindua kampeni hiyo ikiwa ni kauli mbiu yao kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu na wafanyakazi wengine kuzingatia nidhamu muda wote ambayo itaendelea kuchochea maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiwa wanajisomea darasani.
‘Maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi hutokana na mambo mengi ila moja kubwa ni nidhamu ya hali ya juu ambapo shule yetu ndio msingi wake mkuu wa matokeo mazuri kwa wanafunzi wetu, Mwaka jana kati ya wanafunzi 33 ambao walimaliza kidado cha nne wanafunzi 30 walifanikiwa kwenda kidato cha tano’ Akiendelea kufafanua kuhusiana na maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi Mr. Kibona aliwakaribisha wanafunzi wote wanaotaka kujiunga na kidato cha kwanza na kwamba usaili kwa mhula unaokuja umeshaanza. Ambapo utamalizika tarehe 4/ 11/2017. Fomu za kujiunga zinapatikana katika maeneo yafuatayo Shuleni-Boko Basihaya, Msimbazi Center Duka No 19, Tanzania Schools Directory-Sinza, Michele Saloon –Mbezi Beach Africana Kwa maelezo Zaidi ya jinsi ya kujiunga na shule ya John Baptist unaweza kuyapata kupitia tovuti www.johnbaptistsec.co.tz, simu no 0754002900/0754002700

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)