Pages

HOSPITALI YA RABININSIA MEMORIAL YAPEWA HATI YA KUTHAMINIWA NA BENKI YA AZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(kushoto) akimsiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe alipokuwa anazungunza kuhusu namna benki ya Azania inavyowajali wateja wao wadogo wadogo, wa kati na wakubwa na kwenda nao bega kwa bega ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea pamoja nakueleza bidhaa walizonazo katika benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema akizungumza kuhusu changamoto na faida anazozipata kupitia benki ya Azania pamoja na kushauri namna nzuri kuwajali wateja wao mara alipotembelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) ofisini kwake.
  Meneja wa benki ya Azania tawi la Tegeta, Geofrey S. Mahona(kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Azania Bank, Diana Balyagati wakifuatilia mazungumzo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema alipokuwa akisisitiza jambo kuhusu benki ya Azania.


Mkutano ukiendelea wakati wakati wa maofisa wa benki ya Azania pamoja na Mkurugenzi wao walipomtembelea mteja wao ofisini kwake kwa ajili ya kutaka kujua ni changamoto zipi anazipata kwenye biashiara yake. Kushoto ni uongozi wa Hospitali hiyo na kulia ni viongozi wa benki ya Azania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited, Charles Jackson Itembe(kulia) akimkabidhi hati ya kuthaminiwa mteja wa Benki ya Azania Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rabininsia Memorial, Elisania Lema(wa pili kutoka kushoto).
Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)