Pages

Dkt. Kigwangalla atua Loliondo, afanya kikao kizito na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ngorongoro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewasili Makao makuu ya Wilaya ya Ngorongoro na kisha kufanya mkutano maalum na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ambapo kisha atazungukia kwenye maeneo yenye migogoro.

Waziri Dkt.Kigwangalla ametua uwanja mdogo wa Wasso uliopo eneo la Loliondo na kisha kukutana na viongozi hao wa Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka.

Dk Kigwangalla baada ya kumaliza kikao hicho maalum na wakuu hao, anatarajia kutembelea maeneo yenye migogoro ili kubaini kiini cha mgogoro wa eneo hilo la pori tengefu la Loliondo.

Aidha, pia anatarajia kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo pamoja na kufanya mkutano wa wazi ikiwemo kusikiliza kero kutoka kwa wananchi hao.

Waziri Dkt.Kigwangalla yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya sita ambapo awali alianza kutembelea Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)mjini Arusha, na baadae Mamlaa ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia aliweza kukutana na jamii ya wafugaji wanaoishi kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa namna ya kitatua migogoro kati yao na wahifadhi wa Ngorongoro.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea Loliondo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiongozana na na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kwenye uwanja wa ndege wakati akiwasili Loliondo kufuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Rashid Mfaume Taka akimwakilisha Waziri Dk.Kigwangalla katika mkutano huo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)