Pages

Dkt. Kigwangalla atembelea pori tengefu la Loliondo ashuhudia uhalisia wa mgogoro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla mapema jana Oktoba 27,2017 ameweza kutembelea eneo la pori tengefu la Loliondo lililopo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha na kujionea mambo mbalimbali juu ya mgogoro wa muda mrefu maarufu Loliondo.

Waziri Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea katika eneo hilo katika kushuhudia kiini hicho cha mgogoro uliozidi zaidi ya miaka 20, ambapo anatarajia kurejesha majibu kwa Waziri Mkuu pamoja na Rais mara tu baada ya kumaliza ziara yake hiyo pamoja na kukutana na watalaam wake wa Wizara.

Waziri Dkt. Kigwangalla ameweza kuoneshwa eneo lenye mgogoro baina ya mwekezaji pamoja na wananchi wa jamii ya wafugaji kwenye eneo hilo sambamba na kufuatilia mipaka baina ya maeneo mbalimbali yanayozunguka mipaka ya pori hilo tengefu pamoja na hifadhi ya Serengeti.

Awali Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika mkutano wa wazi kwenye Mji wa Wasso aliweza kusitisha operesheni zilizokuwa zinaendelea katika pori hilo tengefu la Loliondo na huku akiagiza mifugo yote iliyoshikiriwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo haijafikishwa mahakamani kuachiwa huru huku ile mingine iliyofunguliwa kesi kuendelea kushikiriwa mpaka shahuri la msingi litakapotatuliwa.

Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla amewataka wananchi hao jamii ya wafugaji katika mgogoro huo kuacha mara moja kuingiza mifugo ndani ya hifadhi licha ya kusitisha Operesheni iliyokuwa ikifanyika na kuwataka wakae meza moja ya majadiriano kupata ufumbuzi.

Akiwa ndani ya pori hilo pia alishuhudia kundi kubwa la wanyama mbalimbali kwenye maeneo hayo ambapo imeelezwa awali hawakuwapo kutokana na kukimbia mifugo iliyokuwa imeingizwa na wafugaji hao.

Waziri wa Maliasili Dkt.Kigwangalla akiwasili eneo la Loliondo kushuhudia kiini cha mgogoro huo
Dkt.Kigwangalla akiwa pamoja na Mbunge wa jimbo hilo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu Mh.Ole Nasha wakati alipofika kukagua kiini cha mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akitazama wanyama eneo lenye mgogoro ambalo ni pori tengefu la Loliondo ambalo awali lilikuwa limevamiwa pamoja na mifugo ya wananchi.
Dkt. Kigwangalla akifuatilia ramani yenye kuonesha eneo la pori tengefu la Loliondo
Baadhi ya wanyama walioonekana wakati Waziri Dkt.Kigwangalla alipotembelea pori hilo ambapo awali wanyama hao walitoweka kutokana na kuingizwa kwamifugo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka (kulia) pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Serengeti William Mwakilema wakati wakikagua maeneo hayo yenye mgogoro huo wa Loliondo.
Dkt.Kigwangalla wakikatisha katika maeneo hayo ya Loliondo wakati akikagua maeneo yenye migogoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa wananchi waliokuwa wakitoa kilio chao kuhusiana na mgogoro huo wa Loliondo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla akizungumza na wananchi jamii ya wafugaji (Hawapo pichaani) wakati alipotembelea eneo la Loliondo ili kubaini kiini cha mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)