Pages

CHAMA CHA WATAALAMU WA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA (CWUVT) CHAANZISHWA KUENDANA NA SERA ZA AWAMU YA TANO

Chama cha Wataalam wa Urembo na Vipodozi Tanzania (CWUVT) wakutana Jijini Dar es salam kwa lengo la kuwakutanisha  pamoja wataalamu wa ngozi, wataalamu wa urembo, wataalam wa saluni,  wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi. Wanachama waasisi wa chama hicho walikutana chini ya Mwenyekiti Mama Shekha Nasser. Dhira ya Asasi hiyo ni kuinua, kuunganisha na kutumikia sekta ya Urembo na Vipodozi, watabibu wa ngozi na wataalamu wa Saluni ambao huboresha maisha ya watu kila siku. Pia kujenga na kudumisha wanachama ambao uwepo wao ni kukuza na kuunga mkono utaalam katika tasnia ya Urembo na Vipodozi kwa ujumla wake. 

Wajumbe waasisi walioudhuria mkutano huo wameipitisha Katiba ya Chama hicho na kuazimia kujitoa na kushirikiana kwa pamoja katika kuelimisha, kuhudumia na kutetea haki za wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi katika tasnia ya Urembo na Vipodozi. 

Chama hicho kimeona jinsi tasnia hii inakua kwa kasi, na mabadiliko ya kitechnologia hivyo wameona ni muda muafaka kwa Watanzania kuwa na uelewa zaidi kuhusu tasnia hiyo kubwa yenye Fursa kubwa ya Ajira hapa Nchini na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi na hata kuingiza mapato ya kigeni.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)