Pages

SOKO KUBWA LA KUUZIA MAGARI YOTE KUANZA DAR KIGAMBONI




Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akionyeshwa eneo na Mkurugenzi wa Property International, Halim Zahran, lililoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya kufanyia biashara ya magari, wakati alipotembelea eneo hilo jana na kuwatangazia rasmi wafanyabiashara wa magari kuanza kuchukua maeneo ambapo watakaa bure kwa muda wa miaka mitatu na baada ya hapo wataanza kulipia. Pia wenye maduka ya vifaa vya magari wametakiwa kuchukua maeneo.

Mafundi wakijenga daraja katika eneo la Viwanda la Kisarawe ii jana.
****************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
MKOA wa Dar es Salaam, unatarajiwa kuanzisha eneo la soko kubwa la pamoja la wafanyabiashara wa magari watakaokuwa katika eneo moja ili kuondokana na wingi na usumbufu wa maeneo ya kuuzia magari hayo katika maeneo ya makazi ya wananchi kwenye mitaa.

Aidha Serikali imepiga marufuku utoaji wa leseni za biashara ya magari katika eneo tofauti na soko holo ifikapo mwaka 2018. Soko hilo ambalo limeanza kuandaliwa na Kampuni ya Property International, katika eneo la Kisarawe II, wilayani Kigamboni litakuwa na upana wa Ekari 2100, sawa na Mita za mraba 750,000.
Kufuatia kujengwa kwa soko hilo, maeneo yote ya kuuzia magari yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya makazi ya wananchi jijini Dar es Salaam yatafungwa na wafanyabishara wote kuhamishia magari yao katika soko kuu hilo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Akipokea eneo hilo kutoka kwa uongozi wa kampuni ya Property Intenational Limited , Mkuu wa mkoa, Paul Makonda, alisema soko hilo litafunguliwa mapema mwakani.
“Biashara ya magari si kama biashara ya Nyanya, kwamba ukihitaji tu unakwenda gengeni kununu, inabidi tuwe na utaratibu kama walivyo wenzetu walioendelea na matunda yake tutayaona, Magari yote hayatauzwa tena nje ya eneo hili. Mtu yoyote akihitaji gari atakwenda Kigamboni, alisema Makonda. 

Aidha alisena kuwa mbali na uuzwaji magari pia kutakuwa na huduma zote za kibiashara kama ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bima, vipuri vya magari, karakana na viwanda vidogo.

Alisema wafanyabishara wanaohitaji kupata maeneo ya kuuzia magari yao watapata maeneo hayo bure na kuyatumia kwa miaka mitatu kisha baada ya ofa hiyo ya miaka mitatu wataanza kulipia gharama ndogo.

“Hili ni eneo kubwa na zuri, litakaloweza kukidhi mipango ya biashara ya magari. Wafanyabishara watapewa maeneo bure kabisa kwa miaka mitatu ila wao wataingia gharama za ujenzi wa uzio kulingana na mahitaji yao, ama kuweka makontena”alisema Makonda.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Property International, Abdulhaleem Zahran alisema, eneo hilo tayari limepimwa na kampuni yake ambalo pia tayari lina eneo la viwanda, na pia kutakuwa na miundombinu yote muhimu na bora.

“Eneo hili litakuwa na miundo mbinu yote bora, hasa ya barabara na kikubwa zaidi ni kwamba liko barabarani hivyo ni rajisi kwa yeyote kufika. Tunaendelea na uboreshaji wa miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa madaraja na barabara za mitaa,”alisema Zahran.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo ya kukagua eneo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International, Abdulhaleem Zahran, akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi akimtembeza Mkuu wa Mkoa katika eneo hilo


Akiendelea kumjuonyesha eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)