Pages

Rwanda yajiimarisha zaidi katika kukuza Lugha ya Kiswahili

Mwenyekiti wa Akademia ya Lugha na Utamaduni Rwanda  Profesa Niyougabo  Cyprien kutoka Kitivo cha Elimu Chuo Kikuu cha Rwanda ,akizungumza leo katika Kongamano la Kiswahili Zanzibar.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus  Zanzibar.

Rwanda inatarajia kuzindua baraza la kiswahili mwaka huu ili kuhimiza matumizi ya lugha nchini humo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Akademia ya Lugha na Utamaduni Rwanda  Profesa Niyougabo  Cyprien kutoka Kitivo cha Elimu Chuo Kikuu cha Rwanda. Kutokana na kupewa hamasa na rais wa nchi hiyo, Paul Kagame ambaye anazungumza vyema Kiswahili.

Aidha amesema kuwa wananchi wa Rwanda wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kujifunza lugha ya kiswahili jambo ambalo linewasukuma kuanzisha  baraza hilo ili kusimamia masuala yanayohusiana na lugha ya kiswahili.

Hata hivyo amesema kuwa matumizi ya lugha ya kiswahili yameimarika nchini humo kutokana na lugha hiyo kufundishwa kuanzia shule za msingi hadi za sekondari

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)