Pages

MKAZI WA YOMBO VITUKA REBECCA AMOS AJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 60 ZA TATU MZUKA

  Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili maisha ya watu,huku akimtaja Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa
Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milio 60,picha shoto ni
rafiki wa mshindi wa Tatu Mzuka kwa wiki hii,Agness Swai


Maganga  alisema kuwa Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya  kupata washindi katika mchezo huu, kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu  Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia  kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao  wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa  washindi mbalimbali nchini Tanzania.”
 Rebecca Amos (pichani kulia),mkazi wa Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha  shilingi milio 60 za Tatu Mzuka,akitoa ushuhuda wake kuhusiana na mchezo huo na hatimaye nae kuibuka mshindi wa mamilioni.Rebecca amewaasa watu  wengine kucheza mchezo huo kwani mmoja wao anaweza akaibuka mshindi na  kubadilisha kabisa mfumo wake wa kimaisha kupitia fedha atakazo kuwa  ameshinda 
Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Rebecca Amos ,mkazi wa  Yombo Vituka aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 60,mapema leo jijini Dar.
Kwa mara nyingine mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, mchezo
unaojinyakulia umaarufu mkubwa nchini Tanzania, umetangaza mshindi wake  wa droo kubwa ya Juma la nane ambaye amejishindia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 60. Mshindi huyu si mwingine bali Bi. Rebecca Amos  mkazi wa Yombo Vituka, jijini Dar es Salaam. 

Bi Rebecca, mwenye umri wa miaka 22, ameibuka na ushindi huu mnono katika  mchezo uliofanyika Jumapili iliyopita na kurushwa mubashara katika  televisheni.

Kufuatia zawadi hii ya iliyotolewa Juma hili na  aina ya washindi wanaoibuka, mchezo wa Tatu Mzuka ni dhahiri umeendelea  kuleta mageuzi makubwa katika eneo la michezo ya Bahati Nasibu hapa  nchini. Hii inatokana na aina ya washindi wanaopatikana na pia uwezo  Tatu Mzuka kutoa zawadi za washindi zinazofikia kiasi cha shilingi  milioni 2 kila saa kwa saa 24 kwa siku. Ushindi huu unatolewa ilhali  kiasi cha kushiriki katika mchezo huu kikiwa ni kuanzia shilingi 500 tu  huku droo za kusaka washindi zikifanyika kila saa.

Akizungumza  na vyombo vya habari kuhusu namna mchezo huu wa Tatu Mzuka unavyobadili  maisha ya watu, Meneja Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga  alisema; “Droo inayofanyika mara moja katika Juma si aina pekee ya  kupata washindi katika mchezo huu kwa kuwa kila mtu anapocheza Tatu  Mzuka anapata pia nafasi ya kushinda mara 200 ya kiasi alichotumia  kucheza kila saa. Droo hizi za kila saa kwa sasa zinatoa washindi ambao  wanapata hadi kiasi cha shilingi milioni 300,000 katika Juma, kwa  washindi mbalimbali nchini Tanzania.”

Bw. Maganga pia aliongeza  kuwa, “tumeongeza kipengele cha ziada katika Tatu Mzuka ambacho kinaitwa ‘Cheza na Washkaji, shinda na washkaji’. Katika kipengele hiki, mshindi wa droo kubwa anapata pia nafasi ya kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao nao hujinyakulia kiasi cha shilingi milioni 1 kila mmoja.”

Bi. Rebecca pia amefanikiwa kutaja majina matatu ya rafiki zake ambao
wamejinyakulia kiasi cha shilingi milioni 1 kila mmoja. Washindi hao wa
ziada wa Bi. Rebecca walikuwa ni mpenzi wake wa miaka mitano Bw.
Ramathan Majiran na marafiki zake wawili tangu shule ya Msingi Agnes na
Amina.  Washindi hawa wa nyongeza nao hawakuamini ushindi wao
hadi pale fedha za ushindi ziliporushwa katika simu zao. Amina alikimbia
kwa furaha kutoa fedha zile na kushangilia akiwa kazishika mkononi huku
Agnes alishangaa kuona fedha hizo zikiingia kwenye simu yake kupitia
MPESA wakati akipata mlo wa mchana. “Nilijawa furaha kubwa sana ambayo  ilinifanya kutoendelea kula,” anasema Agnes.

Bi. Rebecca mshindi wa droo ya nane, ni mama wa motto mmoja ambaye hana ajira kwa sasa.  Anaishi na wazazi wake ambao anawategemea kwa kila kitu.

“Nimekuwa na ndoto, ndoto kubwa tu lakini sikuwahi kuota bkuwa ipo siku
nitafanikiwa kushika fedha nyingi kiasi hiki. Sasa naweza kuanzisha  biashara, kuwasaidia wazazi wangu na pia kuwa na uwezo wa kumhudumia
mwanangu. Kipi cha ziada ambacho binadamu anaomba kupata zaidi ya hiki?” Bi. Rebecca alisikika akisema.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)