Pages

GROUP LA WHATSAPP LA AFYA YANGU LATOA MSAADA KWA WAJAWAZITO KIBAHA MKOANI PWANI

 Msimamizi Mkuu wa Kundi la WhatsAPP la AFYA YANGU, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (kushoto), akimkabidhi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, vifaa vya kujifungulia wajawazito vilivyotolewa na kundi hilo kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi jana. Kulia ni Mwanachama wa kundi hilo, Mudeme Elly.

 Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (katikati), akitoa maelezo wakati akikabidhi msaada huo.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene, akitoa maelezo wakati akipokea msaada huo.
 Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala, akitoa shukurani 
baada ya kupokea msaada huo.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akizungumza wakati akipokea msaada huo.
 Wauguzi wa kituo hicho cha afya wakipiga makofi wakati wakipokea msaada huo.
 Vifaa hivyo vikipokelewa.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akimkabidhi vifaa hivyo Mganga wa Kituo hicho.
 Wauguzi wakipokea vifaa hivyo.
 Baadhi ya majengo ya kituo hicho cha afya.
 Picha ya pamoja.
 Vifaa vikipelekwa kuhifadhiwa.
 Ni furaha tupu baada ya kupokea msaada huo.
Waandishi wa habari wakibadilishana mawazo na Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale. 

Na Dotto Mwaibale, Kibaha

KUNDI la WathAssp la Afya yangu limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 900,000 kwa ajili ya kujifungulia wajawazito kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani.

Vifaa hivyo vilivyopokelewa na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa vilikabidhiwa katika kituo hicho huku tukio hilo likishuhudiwa na Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala na wauguzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Mbunge Jumaa alisema msaada huo umefika kwa wakati muafaka na utasaidia wajawazito katika hospitali hiyo.

"Msaada huu tulioupokea leo hii utawasaidia wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hiki tuna washukuru sana" alisema Jumaa.

Alisema yeye yupo katika makundi ya WathAssap 36 lakini hajawahi kuona yakitoa msaada kwa jamii kama lililofanya kundi hilo la AFYA YANGU ambapo alitoa ushauri kwa makundi mengine kuiga mfano huo.

Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale alisema kama kundi waliguswa na kusukumwa kusaidia katika eneo hilo kufuatia mafunzo ya afya wanayopata kutoka kwa wataalamu wa afya ambao ni wanachama katika kundi hilo.

"Katika kundi letu tuna madaktari ambao hutupa mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya afya ambapo kupitia mafunzo hayo tukasukumwa kuchangishana na kusaidiwa na wadau wengine na kuona tufanye hiki tulichokifanya" alisema Lulale.

Lulale alisema waliona ni vizuri msaada huo kuupeleka nje ya mkoa wa Dar es Salaam ambako wanaamini kunachangoto kubwa ya vifaa hivyo vya kujifungulia kwa wajawazito.

Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene alishukuru kupata msaada huo kutoka katika Group hilo la WhatAssap na kutaka wadau wengine kuiga mfano huo.

Katyene alisema katika kituo hicho cha afya wajawazito 250 hujifungua kwa siku kwa njia ya kawaida huku wanaofanyiwa upasuaji wakiwa kati ya 20 na 25.

Alisema kutokana na hali hiyo licha ya serikali kutoa bure vifaa vya kujifungulia vifaa walivyokabidhiwa na kundi hilo vitasaidia kwa wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)