Pages

WAZIRI WA ARDHI MH.LUKUVI APOKEA RASIMU YA MKAKATI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MATUMIZI BORA YA ARDHI NCHINI, MJINI MOROGORO

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amepokea rarmi Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi bora ya Ardhi Nchini na kutaja Teknolojia kuwa ni changamoto inayokabili mpango wa matumizi bora ya ardhi inayopelekea kulegalega kwa upangaji, upimaji na umikilishaji wa Ardhi.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo mjini Morogoro wakati alipokuwa  akipokea rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi nchini, iliyoonesha na kuainisha mapendekezo katika uandaaji,usimamizi na utekelezaji.

“Tunahitaji teknolojia rahisi ambayo hata ninyi mkondoka serikali inaweza kuhimili, hatupendi mtuambukize teknolojia ambayo itakuwa ni ngumu kwetu, kwakuwa serikali inapopanga gharama kubwa zinajitokeza kwenye picha za anga na zile za chini,” alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema kuwa kuhusu fedha si tatizo lakini ukosefu wa teknolojia ndio tatizo kubwa zaidi,hivyo ni vizuri kuyatazama haya mashirika yasiyo ya kiserikali tushirikiane nayo ili yaweze kuangalia ni teknolojia gani rahisi itakayoweza kupunguza gharama za upimaji na upangaji wa ardhi vijijini baada ya kusubiri ndege za anga ambazo ni gharama kubwa.

Aliongeza kuwa Serikali inapenda kuwa na uratibu wa haraka, ulio rahisi ambao wananchi wanaweza kupanga maeneo yao na kuongeza, lakini pia kuondokana na migogoro ya Ardhi.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akifungua rasmi mkutano kwa ajili ya kusikiliza na kupokea  Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi Nchini, mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Stephen Kebwe akitoa maelezo juu ya mkutano huo na kuonesha namna gani itakavyoweza kumaliza migogoro ya Ardhi Nchini.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi akitoa Mhtasari wa mkutano huo wa kuwasilisha Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi Nchini
 Bw. Gerald Mwakipesile Afisa  Mipango wa Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi akiwasilisha kwa Mh. Lukuvi Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya Ardhi Nchini.
Waziri wa Ardhi Mh. Lukuvi pamoja na wajumbe wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Rasimu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi nchini
 Bw. Emmanuel Msofe kutoka Idara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo na ushiriki wao katika mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya Ardhi
 Bw. Victor Mwita kutoka Wizara ya Kilimo na Ufugaji akichangia jambo ni namna gani watakavyo shirikiana katika kuhakikisha changamoto za Ardhi nchini zinakwisha
 Bi. Bertha Luzabiko Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Morogoro akieleza namna wanavyofanya kazi zao na kushirikiana na watu wa ardhi pia ushiriki wao wa kukabiliana na Changamoto za Matumizi bora ya Ardhi Nchini.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Care Nchini Tanzania Bw. Waleed Rauf akielezea namna ya wanavyoshirikiana vizuri na Serikali kuhakikisha jinsi gani matumizi bora ya Ardhi yanaenda sawa na kuongeza kuwa malengo yao pia ni kuona umasikini unapungua kwa kiasi kikubwa katika jamii zetu.
 Mratibu wa Miradi ya Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akichangia jambo kuwa kupitia rasimu hiyo wadau wamefanya kazi kwa pamoja kuhakikisha sekta ya ardhi ambayo inatambuliwa na wengi wakiwemo  wakulima na wafugaji wadogo wadogo inafanyiwa kazi.
 Bw. Anthony Temu, Meneja wa Ukasimishaji Rasilimali Ardhi Vijijini kupitia Mpango wa Kukasirimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania(MKURABITA) akichangia jambo wakati wa mkutano huo
 Bw. Jamboi Baramayegu Kutoka Ujamaa-CORT akichangia juu ya maswala ya ufugaji na kuomba mkakati huu wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya Ardhi Nchini utambue maeneo ya kulishia mifuko vipindi vyote wakati wa kifukwe na kaingazi pia.
 Kamishna wa Ardhi Nchini Bi. Mary Makondo akichangia jambo na kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na ardhi na kusisitiza ushirikiano wa sekta zote katika kuhakikisha Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi bora ya ardhi unaenda vizuri
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akitoa neno la Shukurani kwa Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za Matumizi Bora ya ardhi na namna Tume itakavyofanya kazi na wadau ili kuhakikisha Mchakato Unafanyika kwa haraka.
 Waziri wa Ardhi Mh. Lukuvi (Kulia) Akikabidhiwa rasmi Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za matumizi Bora ya Ardhi Nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa(Kushoto)
 Waziri wa Ardhi Mh. Lukuvi (wa kwanza kulia) akimkabidhi Kamishna wa Ardhi Nchini Bi. Mary Makondo(wakatikati) Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za matumizi Bora ya Ardhi Nchini, wa tatu kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi.
 Picha ya pamoja baada ya Waziri wa Ardhi Mh. Lukuvi kupokea rasmi Rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Changamoto za matumizi Bora ya Ardhi Nchini
 Wadau wakiendelea kufuatilia Mkutano huo
 Mkutano ukiwa unaendelea.
Picha ya Pamoja Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa Tanzania

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)