Pages

“TPB YASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA JIJINI TANGA”

 Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba Mashingi akizungumza katika Kongamano la Biashara la Jijini Tanga leo
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba Mashingi wa pili kutoka kushoto akifurahia jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamo hilo la Biashara.
AFISA Mtendaji Mkuu wa TPB Benki  Sabasaba Mashingi amewahimiza wafanyabiashara mkoani Tanga kutumia huduma wanazozitoa hususani za mikopo ili waweze kukuza mitaji yao na kutanua wigo wa biashara zao.



Moshingi aliyasema hayo leo wakati akiwasilisha mada katika kongamano la biashara lililofanyika katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga na kufunguliwa na Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe.

Kongamano hilo la biashara ambalo limeandaliwa na Tanzania Standard Newspaper (TSN) katika mkoa wa Tanga lilijumuisha wadau kutoka kwenye taasisi binafsi na za serikali,wafanyabiashara wakubwa na wadogo,vijana na wasomi.

“Niwaambie tu huduma hizo zinatolewa na benki yetu kwa ajili ya wafanyabiashara wa aina mbalimbali lakini pia niwapongeze uongozi wa TSN kwa kuandaa kongamano hilo kwa mara nyengine tena katika mkoa wa Tanga”Alisema.

“Lakini pia nawakaribisha wafanyabiashara wote kutembelea tawi letu la hapa mkoani Tanga lililopo mtaa wa Taifa ili muweze kufaidika na huduma mbalimbali tunazozitoa.


“Kwani Benki yetu ya TPB imejikita kumsaidia mtanzania wa kawaida kuweza kuinua shughuli zake za kiuchumi na hatimaye kukuza uchumi wan chi yetu kwa ujumla “Alisema Moshingi.


Aidha pia alisema wanaunga mkono juhudi kubwa zinazochukuliwa na serikali ya awamu ta tano  kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda ikiwemo jitihada za kufufua viwanda vilivyokufa vikiwemo vya mkoani Tanga.

Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kutumia fursa za mradi wa bomba la mafuta uliozinduliwa na Rais John  Magufuli hivi karibuni kuinua biashara zao kwani wao kama benki wapo tayari kuwasaidia kufikia mafanikio hayo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)