Pages

TCCIA YAANDAA MKUTANO WA PILI WA KIBIASHARA 2017

Makamu wa Rais wa TCCIA Octavian Mshiu akimkabidhi nyaraka ya shukrani Afisa mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Joseph E Haule
Chama cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo (TCCIA)  kimeandaa mkutano maalumu (Business Breakfast) uliowakutanisha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali za serikali wakiwemo TRA, EWURA, BRELA na TBS katika kujadili maswala mbalimbali na muhimu ya kibiashara ikiwemo kuboresha na kukuza ufanisi kwa wanachama wa TCCIA.Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu wa Rais wa TCCIA Octavian Mshiu alisema TCCIA inatambua umuhimu wa ufanyaji kazi wa pamoja na ushirikiano kati ya TCCIA na taasisi za Serikali ili kuleta tija katika biashara hapa Tanzania.
Jackson Lohay kaimu Meneja Mwandamizi huduma za kibenki rejareja Azania BankTukio hilo pia lilimshirikisha mwambata wa biashara wa Uturuki nchini Tanzania Bwana Onur Tekyildiz ambaye alieleza fursa kubwa za biashara kati ya uturuki na Tanzania pia ukuzaji na uvutiaji wa wakezaji na wabia kutoka Uturuki.
Mwambata wa biashara wa Uturuki nchini Tanzania Bwana Onur Tekyildiz
Awali mwakilishi wa Benki ya Azania ilitoa mada juu ya njia za ukuzaji wa baishara na jinsi ya kupata mitaji na fedha za uanzishaji wa viwanda na pia jinsi ilivyojikita katika kuhudumia wateja wa kawaida na wafanyabiashara.Shirika la nyumba la Taifa (NHC) ambao pi walishiriki kikamilifu katika mkutano huo walieleza fursa zilizopo za miradi yake Tanzania kwa wafanyabishara kuweza kumiliki nyumba na ofisi.
Baadhi ya wanachama walishiriki katika mkutao huo 
TCCIA Business Breakfast imeandaliwa na TCCIA pamoja na EAG Group kwa udhamini wa Azania Bank na Shirika la Nyumba la taifa(NHC)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)