Pages

TAARIFA KWA UMMA: DAWASCO KUKATA MAJI KUANZIA AGOSTI 14-19, 2017


TAARIFA KWA UMMA



UBORESHAJI WA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI


BAGAMOYO MKOANI PWANI.

Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wateja wake wote wa Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani kuwa mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini utakuwa kwenye maboresho kwa wastani wa siku 5, kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 14/08/2017 hadi 19/08/2017, hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo kuwa na upungufu wa kiwango cha huduma ya Majisafi.

Sababu ya upungufu wa Majisafi: Maboresho ya Mtambo na mabomba makuu ya usafirishaji na usambazaji Maji.

Maeneo yatakayoathirika: Mji Wa Bagamoyo Vijiji Vya Zinga, Mlingotini, Kilomo na Mapande.

Dawasco inawaomba wateja kutunza Maji ya kutosha kuepuka adha itakayojitokeza.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia: 

Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE) au

Dawati la huduma kwa wateja Dawasco Bagamoyo 0743 451 887

www.dawasco.go.tz 

Imetolewa Na:
Ofisi Ya Uhusiano
Dawasco-Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)