Pages

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC), KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL) ZATILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALINAO YA USHIRIKIANO WA KUTOA HUDUMA

Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, akizungumza na waandishi wa habari, wakati akielezea kuhusu makubaliano ya ushirikiano ya kutoa huduma na Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa. Makubaliano kati ya taasisi hizo, ni katika nyanja za 1. Usafirishaji wafanyakazi, wanaposafiri kikazi, 2.Usafirishaji wa mizigo, vifurushi na barua kupitia ndege za ATCL, 3. Kubadilishana uzoefu wa namna ya kuhudumia wateja, 4. Ushirikiano wa matumizi ya majengo ya Ofisi na 5. Kushirikishana kwenye tovuti kuhusu mambo yote ya Masoko. (Picha zote na KassimMbarouk-www.bayana.blogspot.com
Baadhi ya Maofisa wa TPC na waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, wakati wa mkutano huo. 
Baadhi ya Maofisa wa TPC na waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, wakati wa mkutano huo, wa makubaliano ya ushirikiano wa taasisi hizo wa kutoa huduma.  
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano huo. 
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano huo.  
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa ATCL, Josephat Kagirwa na aliyesimama ni Mwanasheria wa ATCL, Phillipo Mahenge.
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kushoto), wakitia saini mkataba huo wa ushirikiano kati ya taasisi zao hizo. Kulia anayemsaidia Postamasta Mkuu ni Mwanasheria wa TPC, Bi. Zuhura Pinde.
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kushoto), wakitia saini mkataba huo wa ushirikiano kati ya taasisi zao hizo. Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TPC, Elia Madulesi.
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kulia), wakibadilishan hati za mkataba huo, mara baada ya kuusaini jijini Dar es Salaam leo.  
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kulia), wakiuonesha kwa waandishi wa habari mkataba huo, mara baada ya kuusaini jijini Dar es Salaam leo.   
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) akimtambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (wa pili kulia), mara baada ya kumalizika shughuli hiyo, Dar es Salaam leo.  

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)