Pages

SBL yawatunuku magari mawili yenye thamani ya 100m/= wasambazaji wake wa juu jijini Mwanza

Meneja Masoko Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya Serengeti Patrick Kisaka(kushoto) akimkabidhi funguo za gari mshindi wa usambazaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyi Mkurugenzi wa kampuni ya Gramba Stanslaus Mmbaga, wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vinywaji ya Victoria General Supply Jonathan Karaze akipokea ufunguo wa gari kutoka kwa Meneja Masoko Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya Serengeti Patrick Kisaka(kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana baada ya kushinda usambazaji bora.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vinywaji ya Victoria General Supply Jonathan Karaze, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi.

Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji vinywaji  Gramba Stanslaus Mmbaga, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi.

Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL 

Mwanza, Agosti 23 2017- 
Makampuni mawili ya usambazaji vinywaji jijini
Mwanza kila moja yatunukiwa gari kutoka kampuni ya bia ya Serengeti
Breweries Limited (SBL) kwa kuibuka wasambazaji wa juu wa bidhaa zake katika mikoa ya kanda ya ziwa. Makampuni hayo mawili - Gramba Limited kutoka wilaya ya Ilemela na Victoria General Supply Limited kutoka wilaya ya Nyamagana yote yakiwa yamejikita jijini Mwanza

Akikabidhi rasmi magari hayo kwenye sherehe iliyofanyika
kiwandani hapo jijini Mwanza, Meneja wa kibiashara wa kikanda, Bwana Patrick Kisaka aliwapongeza washindi hao wawili kwa kujitolea kwao na kujituma kulikowapelekea kushinda gari hizo aina ya Eicher zenye thamani ya Shilingi 100m/= 
Akitolea ufafanuzi, Kisaka alielezea kuwa Kampuni ya Gramba iliibuka mshindi kwenye kipengele cha uuzwaji wa pombe kali huku Kampuni ya Victoria General Supply ikiibuka mshindi kwenye kipengele cha msingi wa uuzwaji bidhaa.

Baadhi ya bia zitolewazo na SBL ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick. Kampuni pia ni maarufu kwa utoaji wa bidhaa za pombe kali duniani zikiwemo Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain
Morgan Rum pamoja na Baileys Irish Cream. 
“Tunawapongeza washindi kwa jitihada zao zilizowapelekea kuwapiku wasambazaji wengine kwa kanda ya ziwa. Huu ni ushahidi tosha wa kujituma kwao na msukumo wa kufanikiwa kwenye biashara zao” alisema Kisaka akisisitizia kuwa tuzo hizo, za pili kutolewa mwaka huu ni sehemu ya mpango wa robo mwaka wa kutoa msukumo kwa wasambazaji wao.

Akiwatia moyo wasambazaji wengine ambao hawajashinda tuzo hiyo, Kisaka aliwasihi wasambazaji wengine kuongeza juhudi katika kazi zao na
kuwasisitizia kuwa shindano hilo linatoa fursa sawa kwa wote kuweza kujizolea ushindi huku akiwasihi waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano na ushindani katika kufikia malengo waliyojiwekea.

Akitoa salamu zake, Mkurugenzi Mkuu wa Gramba Ltd, Bwana
Stanslaus Mbaga aliwashukuru SBL 
kwa wazo lao la ubunifu lililopelekea kukuwa kwa kasi kwa biashara yake huku akiwasihi wasambazaji wenzake kutoa ushirikiano kwa SBL kwa ukarimu kwa kufanya kazi kwa bidii
 ili kustahili tuzo.

Akiunga mkono maoni ya mshiriki mwenzake, Jonathan Karaze, Mkurugenzi Mkuu wa Victoria General Supply Ltd, pia alishukuru uongozi wa Kampuni ya bia SBL kwa kuanzisha shindano hilo huku akisema kuwa limewasaidia
wasambazaji kufanya kazi kwa bidii zaidi 
Karaze aliwahakikishia SBL juu ya kujitolea kwake katika kukuza zaidi mauzo ya bia ya kampuni hiyo kwakuwa kwa sasa tayari analo gari la usambazaji ambalo litamsaidia kwenye biashara yake hiyo ya usambazaji wa bidhaa zake.

Hii ni mara ya pili SBL inatoa tuzo hizi kwa wasambazaji wake kwa kuchochea majukumu yao ya usambazaji wa bidhaa zao nchini. Mwezi Mei
mwaka huu, tuzo hizo zilitolewa kwa MMG Group, msambazaji mwenye biashara zake wilayani Mpanda mkoani Katavi ambaye alishinda tuzo hizo katika hafla za nusu ya kwanza ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)