Pages

MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao. 
 Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati 


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.

Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.

Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.

Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.

"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti

Wenyeviti hao waliwataka viongozi wa Manispaa ya Iringa kutoa kwa haraka vibari vya ujenzi maana kumekuwa na ukilitimba mwingi kitu kinachosababisha ujenzi holela wa makazi kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa hivyo viongozi wanapaswa kuwa makini na mikakati madhubuti kwa kuwa wananchi wanataka kujenga nyumba zao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa Sweetbert Maro alisema kuwa kweli posho wanazopewa wenyeviti wa mitaa ni ndogo hivyo uongozi wa halmashauri ya manispaa imejipanga kukaa pamoja wenyeviti kujadili jinsi gani ya kuongea posho hizo kulingana na majukumu wanayoyafanya kuiwakilisha serikali.

"Mnafanya kazi kubwa mno lakini mnapewa posho kiduchu hivyo tutakaa na kulijadili hili swala kwa kina kwa kuwa bila wenyeviti wa mitaa halmashauri haiwezi kupata maendeleo na kukuza mji kwa nguvu zote hivyo tunawaomba wenyeviti muendelee kufanya kazi wakati swala la posho linashughulikiwa"alisema Maro

Maro alisema kuwa atamshauri Mkurugenzi kutafuta muda muafaka wa kukaa pamoja wenyeviti wote wa mitaa 192 ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa ili kuzijua changamoto na jinsi gani ya kuzitatua maana leo hii mkutano huu ulikuwa wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.

Aidha Maro aliwataka wenyeviti wa mitaa kuwabana maafisa watendaji wa mitaa maana uongozi wa halmashauri umekuwa ukitoa posho kwa wakati kulingana na agizo la serikali na kufuata sheria ya ugawaji wa posho  kwa walinzi wa amani kwenye mitaa yako.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa kuna kero nyingine atazipeleka bungeni ili kuweza kupatiwa ufumbuzi zaidi na kuzitafutia njia za kuzitatua maana kwa ngazi ya Manispaa wameshindwa kuzitatua.

Kabati aliwaahidi wenyeviti wote wenye kero za ngazi ya manispaa atahakikisha zinatatuliwa kwa wakati lakini amewahakikishia kuwa ataitembelea mitaa yenye kero ambazo zipo kwenye uwezo wake atazitatulia huko huko kwenye mitaa.

Wenyeviti hao walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kuwakutanisha na viongozi wa halmashauri na kusikiliza kero zao kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi ambao utaongeza tija ya kuleta maendeleo kwenye mitaa hao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)