Pages

TPB BANK YAIPA SERIKALI GAWIO LA BILIONI 1

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB Profesa Lettice Rutashobya (kulia) akimkabidhi Hundi kifani yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.032/- Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Phillip Mpango. Gawio hilo limetolewa kwa Serikali baada ya benki hiyo kupata faida ya shilingi Bilioni 15 mwaka jana. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi. Tukio hilo ilifanyika kwenye Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango , Dodoma
 Wakishika kwa pamoja mfano huo wa hundi baada ya makabidhiano.

KWA mara ya kwanza, TPB Bank PLC, jana imetoa gawiwo kwa
Serikali huku Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akionya taasisi za
fedha ambazo zinafanya utatakitishaji wa fedha hazitafumbiwa macho.







TPB Bank PLC ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 86.17 imekabidhi gawio la fedha taslimu la Sh bilioni 1.032 huku
mwanahisa mwingine Shirika la Posta likigawiwa Sh milioni 97 wakati wanahisa wengine
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na na Posta na Simu Saccos zikipewa gawio la
hisa.







Akizungumza
mara baada ya kupokea hudi, Mpango aliipongeza Benki ya TPB kwa 
mafanikio yaliyopelekea kuipatia Serikali gawio hilo kwa mara ya 
kwanza. 






“Niwapongeze kwa mfanikio, niwasihi ninyi kama benki ya
umma mkajitumbukiza kwenye kashafa za kutakatisha fedha. Taasisi zitakazofanya
miamala ya hovyo hvyo hatutasita kuchukua hatua kwa wanaosababisha hasara kubwa
kwa nchi, sasa timetosha.







 Akizungumzia hatua
ya TPB Bank kutoa gawio kwa serikali, alisema inatia moyo kwa taasisi ambazo
serikali imewekeza zikilipa kodi na kutoa gaiwo kwani fedha hizo ndizo
zinazotumika kuwahudumia wananchi.







“Kuna vitu ambavyo havipendezi hata kidogo, watoto wanakaa
chini, kuna wazee ambao wamelitumikia taifa hili, lakini tunashindwa kuwahudumia
hata kwa kutoa matibabu kwa bure, na ni watu ambao kama wao wasingejituma
uwenda sisi tusingekuwepo.







Aidha, Mpango aliutaka uongozi wa TPB Bank kuhakikisha
wanakuja na mfumo wa kusaidia Wanawake na wajasiliamali wadogo kuweza kupata mitaji kwani
ndio makundi makubwa yenye uhitaji mkubwa wa mitaji na kuwa wakiwezeswa wanaweza
kusaidia katika harakati za kukuza uchumi.







“Serikali inadhamira ya kweli katika kuwawezesha
watanzania kiuchumi kwani nia ni kufikia uchumi wa kati si kwa tarakimu bali
utakaogusa moja kwa moja wananchi, hivyo ninyi mnanafasi ya kuwafikia hawa
wajasiliamali ambao ambao ndio wahitaji wakubwa.







Naye Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya
alisema kwa mara ya kwanza benki yake imetoa gawio kwa wanahisa pamoja na kuwa
na tataizo la kimtaji.







“Niliikuta benki inajiendesha kwa hasara, lakini baada ya
mabaliko hayo mwaka 2011 tulianza kuzalisha faida lakini kwa muda wote tulikuwa
tunaomba wanahisa kutumia fadia hiyo kuimarisha mtaji,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)