Pages

Tigo kuungana na wabia wengine kuongeza kasi katika upatikanaji wa Mtandao wa simu kwa wananchi 70,000 katika maeneo ya vijijini Tanzania


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tigo, Simon Karikari akizungumza na waandishi wakati wa mkutano wa kukuza matumizi ya teknologia ya simu ili kufikia maendeleo endelevu uliyoandaliwa na GSMA 360 Afrika, jijini  Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Woinde Shisael. Picha kwa hisani ya Tigo




Tarehe 12 Julai 2015 Dar es salaam - kampuni ya simu ya maisha ya kidigitali  inayoongoza Tanzania, Tigo, Pamoja na wabia wengine, wameshirikiana katika kufanikisha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa watu takribani 70,000 katika maeneo yaliyochaguliwa katika maeneo ya vijijini ya Tanzania.

Ushirikiano na waendeshaji  wengine wa mitandao ya simu (MNOs) (Mobile network Operators), serikali ya Tanzania na Chama cha kutetea maslahi ya waendeshaji wa mitandao ya simu duniani GSMA (Global System Mobile Association), uliundwa kutatua changamoto za upatikanaji wa mtandao katika maeneo ya vijijini kwa kuanzisha maeneo ya majaribio kama sehemu inayokusudiwa ya mradi wa upatikanaji wa mawasiliano.  

Katika ujumbe wake katika kongamano linaloendelea la GSMA la 360 - Afrika lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam leo, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo  Bwana Simon Karikari, alisema kwamba ni kwa kutumia ushirikiano wa sekta ya umma na sekta binafsi ndipo ambapo tunaweza kukabiliana na changamoto za kidigitali, hivyo kukuza mageuzi ya kidigitali ya Afrika.

"Kutoa uunganishaji wa simu wa Broadband kwa jamii za vijijini ni moja kati ya changamoto kubwa ambazo waendeshaji wanakabiliana nazo hapa Tanzania leo. Hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo: Upatikanaji wa Umeme, Mgawanyiko wa watu kijiografia, na uwezo wa kumudu gharama - hata ambapo huduma za data ni moja kati ya huduma za bei nafuu zaidi katika eneo hilo", alisema Karikari. 

Akielezea kuhusu ushirikiano, Karikari amesema kwamba wameingia katika makubaliano ya pande tatu ya roaming ambayo maeneo ya majaribio yatawezesha upatikanaji wa mtandao wa broadband kwa wateja wa mitandao yote kutoka katika mnara mmoja, jambo ambalo litawasaidia watumiaji kutumia mitandao ya kila mmoja wao katika eneo lililochaguliwa.

Mkurugenzi alipongeza ushirikiano wa sekta zaidi ya moja akieleza kwamba ushirikiano huo umewezesha kufanikisha mradi wa roaming wa njia tatu Afrika.

"Kudokeza baadhi tu ya matokeo yetu", Karikari aliongeza kwamba, "Tayari kulikuwa na watumiaji 17,000 wa simu kila siku baada ya uzunduzi. Leo zaidi ya wakaazi elfu 40 wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya 3G kwa mara ya kwanza, idadi inakadiriwa kuongezeka kufikia elfu 70 kufikia mwishoni mwa mwezi Juni 2017).

Akishukuru serikali ya uungaji mkono wake katika kutekeleza mradi huu, Hata hivyo Karikari alisema kwamba, aina fulani ya ruzuku, motisha na makubaliano kama vile kodi katika miundombinu kutoka serikalini, inakaribishwa kusaidia MNOs kupungaza baadhi ya gharama zinazotokana na uanzishaji wa maeneo ambayo hayaja lipwa na mapato yanyotokana na mradi.     



"Tunaamini kwamba mradi huu, pamoja na upekee wake, utaweka uwezekano kwa bara zima la Afrika. Tutaendelea kushirikiana na Serikali, TCRA (Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania), UCSAF (Mfuko wa upatikanaji wa huduma ya mawasiliano Tanzania), na taasisi zingine kutafuta ufumbuzi wa changamoto tulizo zigundua na kuangalia namna tutakavyotumia tuliyojifunza kutoka katika mradi huu kuboresha huduma zetu na hatimaye kuleta uunganisho wa simu Tanzania". Alihitimisha Karikari




No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)