Pages

MAMIA WAFURIKA BANDA LA PSPF MAONESHO YA SABASABA YA 41 JIJINI DAR ES SALAAM

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika kwenye banda la PSPF kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade) kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Wengi wa wananchi hao ni pamoja na wastaafu, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi kuuliza maswali ni jinsi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) unaomuwezsha mtu yoyote aliye kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ili mradi awe na kazi
inayomuinguizia kipato.

Akijibu maswali ya waliohitaji kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, Meenja wa Mpango huo, Bi. Mwanjaa Sembe alisema, kujiunga na mpango hyuo ni bure na mtu atakayejiunga atahitajika kuchangia shilingi kiwango chochote kila mwezi ambapo kiwango cha chini kabisa ni shilingi elfu kumi (10,000) tu. Alisema mpango wa uchangiaji wa hiari licha ya kumuwezesha mwanachama kujiwekea akiba yake, lakini pia anafaidika na mafao mbalimbali ikiwemo fao la bima ya afya. Fao la elimu, fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kujitoa na mikopo ya nyumba na viwanja, haya yote yatategemea na jinsi unavyojiwekea akiba (michango)
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kushoto), akipokea zawadi ambayo ni taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa Hiari, 9PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, wakati alipotembelea banda la Mfuko huo Julai 1, 2017. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha Mnyamani. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.
 Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha Mnyamani, (kushoto), akimuhudumia mwananchi.
Afisa wa Polisi aliyefika kujua michango yake akipatiwa huduma na Afisa uendeshaji wa PSPF, Bw.Miteko Chaula.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)