Pages

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOTEMBELEA BANDA LA ASAS KWENYE MAONESHO YA BIASHARA YA SABASABA KILWA ROAD JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye banda la bidhaa zitokanazo na maziwa la Kampuni ya ASAS, viwanja vya Kimataifa vya Maonesho ya Biashara (Sabasaba), Kilwa Road jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kampuni hiyo, kwenye banda hilo la bidhaa zitokanazo na maziwa. Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Kulia ni Mkurugenzi wa ASAS, Bw. Faraj Jaffar Abri.
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa zawadi Maneja wa Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi wa Mamaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bw. Christopher Chizza.
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akipatiwa maelezo kuhusu masuala ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na Maneja wa Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu. 
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiwa ameishikilia moja ya tuzo ilizoshinda kampuni hiyo kutokana na ubora wa bidhaa zake. 
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiiangalia tuzo hiyo, huku Maneja Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu (kulia), akisubiri kumkabidhi tuzo nyingine ilizoshinda kampuni hiyo kutokana na ubora wa bidhaa zake. 
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akiiangalia tuzo hiyo, mara baada ya kukabidhiwa na Maneja Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Maneja Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu (kulia), akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kuhusu tuzo hiyo. Anayeangalia kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Maneja Masoko na Matukio wa Kampuni ya ASAS, Jimmy Kiwelu (kulia), akimweleza Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jinsi kampuni hiyo, ilivyofanikiwa katika kupiga hatua za maendeleo katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa.
Maneja Masoko na Matukio wa Kampuni ya ASAS, Jimmy Kiwelu (kulia), akimweleza Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jinsi kampuni hiyo, ilivyofanikiwa katika kupiga hatua za maendeleo katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa. 
Maneja Masoko na Matukio wa Kampuni ya ASAS, Jimmy Kiwelu (kulia), akizidi kumfafanulia Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan jinsi kampuni hiyo, ilivyofanikiwa kwa kiwango cha juu katika uzalishaji wa bidhaa hizo, zitokanazo na maziwa. 
Makamu wa Rais, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akimweleza jambo Maneja wa Masoko na Matukio wa kampuni hiyo, Jimmy Kiwelu kuhusu katika kuwaendeleza wananchi katika uzalishaji wa bidhaa hizo pamoja na kuwapatia mitamba kwa ajili ya kujikwamua kimaisha. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)