Pages

BALOZI DK.PINDI CHANA NA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI WA LAPF WATEMMBELEA BANDA LA LAPF MAONYESHO YA SABASABA

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akisalimiana na  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam,mapema jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya LAPF Prof. Faustine  Bee (katikati aliyeshika tuzo ya ushindi wa Lapf )akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa LAPF Bw.James Mlowe   pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati alipotembelea  banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF katika viwanja vya Sabasaba mapema jana .
Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa mtumishi wa LAPF Simboninsia Ndosi  alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe mapema jana
Wanachama wapya wa LAPF wakielekezwa kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika viwanja vya sabasaba mapema jana.

Mtumishi wa LAPF  akimsajili  mmoja wa wanachama wa  LAPF alietembelea banda hilo.

Wateja wakiwa wanasubiri kupata kadi zao za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika maonesho ya sabasaba.
Maafisa wa LAPF wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye banda la LAPF na kujiunga na uanachama kwenye mfuko katika maonesho ya SabaSaba mapema jana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)