Pages

WANAWAKE WA KANISA LA PENTEKOSTE TANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA KUDUMISHA AMANI NCHINI

Naibu  Katibu Mkuu wa  Muungano wa Makanisa ya Pentekoste katika Tanzania wa Umoja wa Wanawake (UW-MMPT), Loveness Maiko akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa kanisa hilo la mwaka huu wa 2017 lililofikia tamati jana Misheni ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

 Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Kitaifa, Erasto Makalla akitoa mahubiri ya kufunga kongamano hilo.
 Askofu Methusela John Mpera akiongoza maombi ya kufunga kongamano hilo.
 Hii ni kamati nzima iliyofanikisha kongamano hilo.
 Taswira ya kongamano hilo. Hawa ni wanawake walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali.
 Kwaya ya Praise Team ikitoa burudani kwenye kongamano hilo.
 Mwenyekiti wa UW-MMPT, Jaqueline Ezekiel (kushoto), akimkabidhi zawadi Askofu Mkuu wa Kanisa hilo hapa nchini, Erasto Makalla.
 Mwenyekiti wa UW-MMPT, Jaqueline Ezekiel (kushoto), akimkabidhi zawadi, Askofu Obedi Fabian wa Kanisa hilo Zanzibar. Wa pili kulia ni mke wa Askofu huyo, Ruth Obedi.

 Zawadi zikiendelea kutolewa.
 Hapa ni Mwenyekiti wa UW-MMPT na Makamu Mwenyekiti wakifurahi kumalizika kwa kongamano.
 Ni furaha baada ya kupokea zawadi.
 Hapa ni kumtukuza mungu kwa kucheza nyimbo za sifa.
 Ni kuserebuka kwa kumsifu mungu kwa kufanikisha 
kongamano hilo.
Mikono juu kwa furaha 

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE wa Kanisa la Pentekoste Tanzania wametakiwa kushirikiana na kudumisha amani iliyopo nchini ili waweze kuabudu na kufanya shughuli zao za maendeleo.

Mwito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania Misheni ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Methusela Mpera wakati akitoa salamu za kufunga kongamano la wanawake la kitaifa la Muungano wa Makanisa ya Pentekosti katika Tanzania UW-MMPT jana.

"Ni wajibu wenu wanawake kushirikiana, kushikamana na kudumisha amani iliyopo nchini ili muweze kufanya shughuli zenu za maendeleo na kuabudu" alisema Askofu Mpera.

Alisema wanawake ni chachu ya maendeleo katika kanisa na taifa hivyo wanakila sababu ya kushikamana badala ya kufikiria mambo yasiyo mpendeza mungu kama  majungu na mengineyi ambayo hayapaswi kuandikwa au kuongelewa mbele ya kanamdasi.

Akizungumza wakati akitoa mahubiri ya kufunga kongamano hilo Askofu Mkuu Wa kanisa hilo nchini, Erasto Makalla aliwataka waumini wa kanisa hilo kuwa na imani ya kweli badala ya kuwa na imani ya nusu nusu.

Alisema safari ya mbinguni sio nyepesi kama wanavyoweza kufikiri bali ni ndefu ambayo inahitaji mtu mwenye imani ya kweli na mwenye upendo kama maneno ya mungu yanavyoeleza.

Makalla aliwataka waumini wanapokuwa katika mfungo wa maombi kuacha kufunga kwa siku nyingi bila ya kula wala kunywa maji kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha maisha yao.

"Mnapofunga kwa muda mrefu bila ya kula msiache kunywa maji japo kidogo badala ya kuacha kabisa kula chochote kwa kufanya hivyo mnaweza kupoteza maisha yenu" alisema Askofu Makalla.

Katika kongamano hilo yalifanyika maombi ya kuliombea kanisa hilo, taifa na Rais Dk.John Pombe Magufuli ili aendelee kuongoza nchi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)