Pages

WANAWAKE VIONGOZI KATIKA MASOKO WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUTEMBELEA KATIKA MASOKO AONE MIUNDOMBINU ILIVYO

Ofisa Mradi wa 'Mpe Riziki Si Matusi' kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), Suzan Sita (kulia), akitoa mada katika Warsha ya Siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa Umoja wa Wanawake Masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na shirika hilo inayoendelea katika Hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam jana.
Viongozi hao wakiwa katika warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Warsha hiyo. Kulia ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Irene Daniel.
Taswira katika ukumbi wa mikutano.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas, akichangia mada. (kulia) ni Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma na kushoto ni Verdiana Gervas kutoka Soko la Ilala.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Ilala Mchikichini, Bupe George akichangia mada.
Mwezeshaji Sheria wa Soko la Kigogo Kisambusa, Mariam Rashid akichangi mada.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele akichangia jambo.

Mfanyabiashara kutoka Soko la Gongolamboto, Elika Mwakyusa akichangia.
Mwezeshaji Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Johanitha Katunzi akichangia mada.
Mshiriki wa warsha hiyo  akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akichangia jambo.
Mwezeshaji Sheria kutoka Soko la Kiwalani Kigilagila, Bisura Juma akichangia jambo.


Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI Wanawake katika masoko jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk.John Magufuli atembelee masoko wanayofanyia shughuli zao ili aone changamoto ya miundombinu katika masoko hayo.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mwezeshaji wa Sheria katika Soko la Ilala Mchikichini, Consolata Cleophas  wakati akichangia mada kwenye warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa umoja wa wanawake masokoni iliyohusu ukatili dhidi ya wanawake na haki zao iliyoandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)

Alisema wafanyabiashara wakiwemo wanawake wamekuwa wakilipa ushuru kila siku katika masoko hayo lakini manispaa husika zimeshindwa kuwajengea miundombinu kama vyoo bora, umeme na maji hivyo kuwa changamoto kubwa kwao.

"Tumekuwa tukitoswa ushuru wa shilingi 500 kwa siku kwa kila mfanyabiashara lakini hatuoni jitihada zozote zinazochuliwa na hizi manispaa zetu za kutuwekea miundombinu bora ndio maana tunamupomba Rais wetu afanye ziara katika masoko tunayofanyia kazi ili tuzungumze naye na kuiona changamoto hii tuliyonayo" alisema Cleophas.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wafanyabiashara masokoni Tanzania, Betty Mtewele alisema wakati ufike manispaa ziweke wazi sheria ya ulipaji wa ushuru kwa mfanyabiashara ambaye hakufika sokoni kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kuumwa kwani anapo pona na kurudi katika eneo lake la kazi anatakiwa kulipa ushuru wa muda huo wote ambao hakufanya biashara wakati alipokuwa akijiuguza.

"Tunaomba manispaa zetu ziweke wazi jambo hili kwani limekuwa ni changamoto kubwa sana kwetu" alisema Mtewele.

Mwezeshai wa Sheria katika Soko la Kigogo Sambusa Mariam Rashid alisema zabuni za uzoaji taka katika masoko zinapaswa kuangaliwa kwa karibu kwani wengi wanaozipata hawana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo kusababisha masoko mengi kuwa na changamoto ya mlundikano wa takataka ambapo alishauri kuondoa mfumo dume katika masoko unaotoa tenda hizo na badala yake zitolewe fursa kwa wanawake ili waweze kuingia katika kamati za masoko ili nao waweze kuchangia katika mambo mbalimbali.

Elika Mwakyusa aliomba manispaa ya Ilala kutenga eneo la soko Gongolamboto ambako hakuna soko kwani eneo wanalofanyia biashara zao ni la mtu binafsi hivyo wamekuwa na changamoto kubwa ikiwemo kumlipa ushuru mkubwa mtu huyo.

Mwezeshaji sheria wa Soko la Vingunguti wa Simba, Maimuna Mungi alisema ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi mbalimbali katika soko hilo hakuna kutokana na kuwepo kwa mfumo dume jambo ambalo limechangia wanawake wafanyabiashara katika soko hilo kushindwa kuzipatia kusaidiwa changamoto walizonazo.

Mwezeshai Sheria kutoka Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa aliomba asilimia 10 ya fedha za makusanyo ya ushuru zibaki katika masoko husika ili zisaidie ujenzi wa miundombinu.

Ofisa Mradi wa Mpe Riziki si Matusi kutoka EfG Suzan Sitha alisema lengo la warsha hiyo ni kuwaongezea uelewa viongozi wanawake masokoni kuhusu ukatili dhidi yao pamoja na kupanga mikakati ya kuendeleza kampeni za kupunguza ukatili dhidi ya wanawake masokoni baada ya mradi kuisha.

Alitaja lengo lingine ni kutambua haki za wanawake na wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake pamoja na kuwakumbusha viongozi juu ya wajibu wao na utunzaji wa kumbukumbu za vikundi.

Sitha alisema warsha hiyo imewashirikisha viongozi wanawake kutoka masoko  ya Manispaa ya Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam, ambayo ni Ilala Boma, Gongolamboto, Mombasa, Kiwalani, Mchikichini, Kigogo Fresh, Kigogo Sambusa, Chamazi, Kiustu, Kinyerezi, Feri, Temeke Sterio, Buguruni, Gezaulole, Tabata Muslim na Vingunguti kwa Simba.

Alisema karibu changamoto zote zilizopo katika masoko zinalingana kubwa ikiwa ni miundombinu mibovu licha ya  wafanyabiashara kulipa ushuru na kuwa mradi huo wa Mpe Riziki Si Matusi upo katika Wilaya ya Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ambapo mradi mkubwa wa Sauti ya Mwanamke Sokoni  upo katika mikoa tisa hapa nchini.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)