Pages

UPDATES MSIBA WA MAREHEMU BALOZI CISCO MTIRO, MAZISHI KUFANYIKA JUMATANO


Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo


Jioni hii Bw. Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 

Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.

Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.

 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.


Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)